Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wanawake (UN-Women) kila siku takribani wasichana 39,000 elfu kuolewa kabla ya umri wa miaka 18 duniani.

Akizungumza katika sherehe za kumaliza elimu ya sekondari kwa wajumbe wa klabu za Umoja wa Mataifa kwa vijana, Youth of United Nations Association of Tanzania (YUNA) Mgeni rasmi kwenye sherehe hizo, Stephanie Raison, Afisa habari kutoka shirika la Umoja wa Mataifa Wanawake (UN-Women) alisema kwamba kama tatizo hilo la ndoa za utotoni likiendelea zaidi ya wasichana 140 millioni watakuwa wameolewa ifikapo 2020.
Takriban wasichana milioni 14 million kote duniani wanalazimishwa kuolewa wakiwa wadogo
“wasichana wanaolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 18 wapo katika hatari ya kunyanyaswa  kufanyiwa ukatili wa kijinsia na wanaume wao na kupata matatizo yatokanayo na uzazi wakati wa kujifungua ikiwemo kupoteza maisha katika umri mdogo,” alisema Raison 

Alisema kwamba kuondoa ukatili wa kijinsia kwa watoto wa kike duniani ni moja ya agenda ya muhimu katika mkutano uliofanyika mjini Beijing wa wanawake katika kumsaidia mwanamke na mtoto wa kike kuondokana na unyanyasaji wa kijinsia duniani kote.
Umaskini ndio sababu kubwa ya wasichana kuolewa mapema
Bi Raison alisema kwamba ahadi ya jumuiya ya kimataifa katika mkutano wanne wa kidunia wa wanawake mjini Beijing ni kuondoa kabisa aina zote za ukatiki wa watoto wa kike na wanawake katika nchi hasa zinazoendelea.

“katika mkutano uliopita wajumbe walikuabaliana kuondoa ainza zote za ukatili wa kijinsia na kutafuta njia bora ya kuwakinga watoto wa kike dhidi ya unyanyasaji wa aina yoyote na kuhakikishia elimu na malezi bora kwa watoto kike duniani,” aliongeza
Aliongeza kwamba jumuiya ya kimataifa ipo katika mpango mkakati wa kusukuma katika umuhimu na ulazima wa elimu kwa mtoto wa kike na afya bora ya uzazi ili kuwajengea mazingira ya kuwa viongozi na wakinamama bora baadaye.

Bi Raison alisema kwamba ni muhimu kwa serikali zote duniani kushirikiana na Umoja wa Mataifa wanawake katika kuhakikishia wanajenga usawa wa kijinsia kati ya watoto wa kike na kiume kama njia bora ya kuleta maendeleo kwenye jamii.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Klabu za Umoja wa Mataifa kwa Vijana, Bi Caroline Damian alisema kwamba kila mwaka klabu za umoja wa mataifa kufanya sherehe kwa wajumbe wake ili kuleta hamasa ya vijana kujitambua na kutambua wajibu wao kama vijana.

Alisema kwamba masuala ya afya ya uzazi, mimba za utotoni na ndoa ni changamoto kubwa kwa vijana na hasa watoto wa kike hapa nchini Tanzania na dunia kwa ujumla.

Alifafanua kwamba ni wakati kwa jumuiya ya kimataifa kutoa elimu ya kutosha kuhusu afya ya uzazi kwa vijana na umuhimu wa elimu ili kupunguza tatizo la ndoa na mimba za utotoni pamoja na vifo.
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.