Serikali imeamua kuanzisha
usajili mpya wa namba za pikipiki (aina zote za pikipiki zenye
magurudumu mawili na zaidi) ili kurahisisha usimamizi na utawala wa
vyombo vya moto. Utaratibu mpya wa Usajili unaanza rasmi tarehe
1/10/2014. Mmiliki anapewa muda wa miezi sita kubadilisha usajili bila
adhabu.
Pikipiki za magurudumu mawili |
Usajili huu utahusu vyombo vya moto aina ya pikipiki vyenye magurudumu mawili au zaidi. Pikipiki kwa ajili ya biashara zinatakiwa kubandikwa vibao vya namba ya rangi nyeupe na kwa ajili shughuli binafsi zitabandikwa vibao vya namba za rangi ya njano.
Usajili huu utafanyika katika ofisi zote za TRA na mmiliki anatakiwa kwenda TRA na kadi halisi ya pikipiki na Tshs.10, 000/- kwa ajili ya kadi mpya.
Wito unatolewa kwa
wamiliki wote wa pikipiki ikiwa ni pamoja na zile za magurudumu matatu
au manne maarufu kwa jina la Bajaji, wafike katika ofisi za Mamlaka ya
Mapato Tanzania kwa ajili ya kukamilisha usajili wa vyombo
wanavyomiliki.
Vyombo vya usafiri vya magurudumu matatu almaarufu kama Bajaj |
Post a Comment