Kampuni hiyo ya ina maelfu ya wafanyakazi kutoka India
Na Mwandishi Wetu,
Mamlaka ya Kazi nchini Marekani imeipiga
faini kampuni ya Silicon Valley kwa kosa la kulipa mishahara wafanyakazi wanane
kutoka India isivyo stahiki “grossly underpaying” kwa mujibu wa sheria za kazi
na mahusiano kazi nchini marekani
Eneo la bonde la Silicon ambapo jamii wengi ta watu toka India wanafanya kazi |
Kampuni yenye makao yake makuu jijini
California inayojishughulisha na vifaa vya umeme imepigwa faini kwa kulipa
kiasi cha Dola 1.21 kwa saa moja na wafanyakazi hao wanafanya kazi kwa masaa
122 kwa wiki bila malipo baada ya muda rasmi wa kazi.
Kampuni hiyo inasema kwamba ni kwa bahati
mbay tu waligafulika “overlooked” kwa
sheria za kazi na viwango vya mishahara baada ya muda rasmi wa kazi na viwango
vya mishahara vilivyowekwa na mamlaka ya jiji hilo la California ni Dola 8 kwa
saa.
Maelfu ya wafanyakazi kutoka India wanafanya
kazi kwenye kampuni hiyo ya Silicon Valley na wengi walianzia kazi hapo.
Ripoti imesema kwamba kampuni hiyo ya
vifaa vya umeme, na ya uchapishaji wa kutumia teknolojia, wanatakiwa kulipa
zaidi ya Dola za kimarekani 43,000 katika mishahara na faini kutoka katika
kanuni za ajira kwa ukiukwaji wa taratibu.
Wafanyakazi hao nane walipelekwa nchini Marekani
kwenye miradi maalum, na katika wakati waliposaidia kwa kampuni hiyo kuhamisha
makao makuu yake kutoka mjini wa foster hadi Fremont.
Ripoti imesema zaidi kwamba kampuni hiyo
walikuwa wakiwalipa wafanyakazi hao kutoka India mishahara sawa na waliokuwa
wakilipwa wakati wakifanya kazi kutoka kwenye jiji la Bangalore.
Sheria za Marekani zinataka wafanyakazi
wote kutoka nje walipwe mishahara kwa viwango vilivyowekwa na sheria za kazi na
mishahara za nchi hiyo na malipo baada ya muda rasmi wa kazi wa masaa 40 kwa
wiki.
“hii ni mbaya sana kupita kitu chochote
sijawahi kuona katika sheria za Marekani na hapa katika jiji la Los Angeles,”
amesema Michael Eastwood, Naibu Mkurugenzi wa Wilaya katika idara ya Ajira,
aliliambia Shirika la Habari la Associated Press.
Post a Comment