Lorraine Clement akipungia watu waliofika kumlaki , alipokuwa akiwasili uwanja wa ndege JNI, alipokuwa akitokea nchini, Thailand, kushiriki mashindano ya Miss Grand International 2014, ambapo Lorraine aliibuka nafasi ya 20 bora. |
MWANADADA Lorraine Clement aliyeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya
urembo ya kimataifa ya Miss Grand International 2014, na kufanikiwa
kushika nafasi ya 20 bora katika shindano lililofanyika mjini, Bangkok,
Thailand, ametua nchini jana Oktoba 9 majira ya saa 10 jioni na
kuwashukuru watanzania kwa kumuunga mkono.
Akizungumza na wandishi wa habari muda mfupi alipowasili uwanja wa ndege
wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es Salaam, Lorraine aliwashukuru
wadau mbalimbali kwa kufanikisha ushiriki wake kwenye mashindano hayo makubwa
duniani, ikiwemo kampuni ya Redline Communication Ltd,
Iliyofanikisha mshiriki huyo kushiriki kwa mwaka huu.
“Pongezi kwa wadau wote mliofanikisha mimi kupeperusha vyema
bendera ya Tanzania. Millen Magese kupitia kampuni yake ya MMG,
Jacqueline Kibacha, Doreen Mashika, Husna Tandika na wengine wengi.
Katika mapokezi hayo, Lorraine alilakiwa pia na wazazi wake pamoja
na mtendaji Mkuu wa Redline Communication, Abubakar Faraji ‘Abu’ na wadau
wengine walijitokeza uwanjani hapo.
Kwa upande wake, Mama Mzazi wa Lorraine, Paula David aliwashukuru
watanzania kwa kumpigia kura mwanae na kupeperusha vyema bendera ya Tanzania.
Hii ni kwa mara kwanza, mtanzania huyo anashiriki shindano hilo ambalo
kwa hapa nchini linaendeshwa na kampuni ya Redline Communication Ltd,
ambapo mshiriki wake huitwa ‘Miss Grand Tanzania’, kwa mwaka huu,
Lorraine alikuwa ni mshindi wa pili kwenye shindano la Tanzania Top
Models 2013.
Aidha, Katika shindano hilo, mwanadada, Daryanne Lees kutoka nchi ya
Cuba, ndiye aliyetwaa taji hilo kwa mwaka huu. Wengine ni Miss Ethiopia, Hiwot
Mamo na Miss Canada, Kathryn Kohut.
Shindano hilo la Miss Grand International, kwa sasa ni msimu wa pili
likifanyika nchini Thailand, tokea kuanzisha mwaka 2013. Mshindi wa mwaka huu,
ameweza kunyakua kitita taslimu cha dola za kimarekani 40,000, pamoja na
thamani za ndani.
Lorraine Clement akishukuru Mungu, alipokuwa akiwasili uwanja wa ndege JNI, alipokuwa akitokea nchini, Thailand, kushiriki mashindano ya Miss Grand International 2014, ambapo Lorraine aliibuka nafasi ya 20 bora. |
Lorraine akilakiwa na meneja wake Abubakar Faraji |
Lorrainea kiwa na familia yake na mama yake (kulia). |
Post a Comment