Blogu ya Daniel Mjema inataarifu kuwa jana kituo kikuu cha mabasi yaendayo sehemu mbalimbali ndani ya mkoa wa Kilimanjaro kiligeuzwa kuwa kiwanja cha kabubmbu baada ya madereva na utingo kugoma kutoa huduma.
Kutokana na stendi kuwa tupu, madereva wakaunda na makondakta hao wakaunda timu mbili na kuanza kucheza soka isiyo rasmi huku abiria wakilazimika kupakia magari ya kusafirisha magazeti, pikipiki, magari madogo ya wazi n.k. ili kufanikisha safari zao.

Habari kamili na picha zaidi vimepachikwa hapo chini...









MAGARI yanayofanya safari zake katika Barabara ya Moshi-Arusha zimegoma kufanya safari kwa takribani masaa 9 yakipinga kulipishwa bondi ya makosa ya shilingi elfu 30 katika kila kituo kwa kosa lilelile.


Wakizungumzia chanzo cha mgomo huo, baadhi ya wamiliki na madereva wa magari yaendayo, Marangu, Rombo, Arusha, Rau pamoja na magari yote yanayotoa huduma katika maeneo ya mijini kama vile pasua KCMC na Uru, wamesema sababu ya msingi ya kufanya mgomo huo kulishinikiza kitengo cha usalama barabarani na Mamlaka ya usafiri wa majii ya nchi kavu (SUMATRA), kuangalia upya tozo hizo.

Akizungumza kwa niaba ya madereva hao, katika kikao kilichoitishwa na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, na kukutanisha pande zote kwa maana ya Akiboa, Jeshi la Polisi na SUMATRA, Mwenbyekiti wa Akiboa kanda ya Kaskazini, Hussein Mrindoko, amesema kiini cha mgomo huo ni kitendo cha udhalilishaji wanaofanyiwa na askari wa usalama barabarani.

Kwa upande wake Mkuu wa kituo kidogo cha polisi Moshi mjini OCS, Hendry Nguvumali anayelalamikiwa kulazimisha faini kinyume cha sheria, pamoja na kufanya kazi akiwa mlevi amesema malalamiko yote yametokana na ukweli kwamba anafanya kazi kwa mujibu wa sheria za Jeshi la polisi.

Akijibu malalamiko yaliyolekezwa kwa SUMATRA kuhusu ucheleweshaji wa stika na ukamataji wa leseni za biashara ya usafiri, Meneja wa mamlaka hiyo mkoa Kilimanjaro Fabian Nyang’oro amesema SUMATRA imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa mujibu wa taratibu na sheria za usalama barabarani pamoja na sheria ya umiliki wa vyombo vya usafiri.

Amesema endapo mmiliki wa Chombo cha biashara ya usafiri atakiuka sheria hizo wao kama wasimamizi kazi yao sio kukamata magari bali kuhakikisha stika ambazo zimechukuliwa kinyume cha taratibu wa utoaji wa leseni za biashara zinafutwa.

Naye Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama, alisema kimsingi tatizo hilo halikutakiwa kuwepo maana taratibu zote za kisheria ziko wazi ambapo aliitaka SUMATRA kama wenye dhamana kuu na usafiri barabarani kuhakikisha wanakaa meza moja na Jeshi la Polisi pamoja na Akiboa kuzungumzia malalamiko yote yaliyowasilishwa na kuyapatia ufumbuzi.

Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani hapo, Robert Boaz, aliwataka Madereva kufuata sheria na kuwataka kuacha kulalamika ambayo kimsingi wanayasababisha wao kutokana na kukiuka taratibu za usalama barabarani.

Amesema baada ya kutolewa kwa taarifa ya Mkoa wa Kilimanjaro kuwa ya pili kwa ajali za barabarani, Jehsi la Plisi mkoani hapo lilichukua hatua ya kuhakikisha inakabiliana na tatizo hilo ambalo alisema kwa asilimia kubwa husababishwa na uzembe wa madereva wawapo barabarani.


 

 

 
 
 

 

 

 

Aisee Mangi twende huku

 

 

 

 

Chanzo cha habari toka mtandao wa  www.wavuti.com






























































Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.