Na Damas Makangale, MakangaleSATELLITE Tanzania 

 KAMPUNI ya Saruji ya Tanga (TCCL) kupitia bidhaa yake ya Simba Cement imesema itaendelea kudhamini  mshindano ya kila mwaka ya Kilimanjaro Premium Lager Kilimanjaro Marathon yanayofanyika mjini Moshi  Mkoani Kilimanjaro.

 
Akizungumza muda mfupi mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya mwaka huu katika uwanja wa MUCCOBS mjini Moshi juzi, Meneja Biashara wa Tanga Cement, Hamish Frazer amesema kampuni yake itaendelea kudhamini mashindano hayo mwakani mara baada ya kwisha kwa mkataba wa udhamini wa miaka miwili mwaka huu.
Amesema Simba Cement inajivunia kuingia mkataba wa Dola za Kimarekani 17,000 kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita ikitoa udhamini wa kituo cha viburudisho na maji kwa ajili ya kupooza joto kwa wakimbiaji.
"Mbali na udhamini huo kila mwaka Simba Cement inadhamini pia wafanyakazi wake kushiriki katika mbio hizo, mwaka  huu ikitumia zaidi ya shs milioni 20 kudhamini wafanyakazi wake 35", akaongeza.
Akizungumzia mashindano ya mwaka huu, Mkurugenzi Mtendaji wa Simba Cement, Reinhardt Swart amesema Kilimanjaro Marathon ni moja matukio yanayopewa umuhimu katika orodha ya matukio katika kampuni yao.
"Tunafurahi sana kushiriki mbio hizo katika mazingira ya kuvutia chini ya Mlima Kilimanjaro na huku tukijivunia  kuwa sehemu ya wafanikishaji wa tukio hili lililo katika kalenda ya matukio muhimu hapa nchini", akaongeza.
Mkurugenzi huyo ambaye ameshiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza mwaka huu toka alipochaguliwa kushika nafasi  hiyo alisema yeye binafsi angependa washiriki wengi zaidi kutoka nje ya nchi waje kushiriki mwakani.
"Ni matamanio yangu Kilimanjaro Marathon izidi kuwa kubwa na kupata umaarufu zaidi kuliko hata ule wa  mashindano ya New York Marathon", amesema.
Simba Cement ilianza kudhamini mbio hizi tokea mwaka 2003 ambazo mdhamini wake mkubwa  ni kampuni ya Bia ya TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager mwaka huu yakishirikisha wakimbiaji zaidi ya 6000 kutoka ndani na nje ya nchi.
MWISHO.

 

 

 

 




 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.