Tigo Tanzania mkombozi wa wanawake wajasiriamali nchini
Mwaka jana walizindua mpango wa Wezesha
Wanawake kwa Maendeleo
Wanawake wengi sasa wameweza kujiendeleza
kibiashara na kuhudumia familia zao kwa ubora zaidi.
Na Damas Makangale, Tanzania
JUMAMOSI ya kesho, Tanzania itaungana na
nchi zingine duniani kuadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake ambapo shughuli
mbalimbali zitafanyika katika kutambua mchango wa wanawake kuanzia ngazi ya
kaya, taifa na kimataifa.
Siku ya wanawake duniani ni siku ya
kimataifa na dunia nzima huadhimisha siku hii ya kipekee kwa kufurahia
mafanikio yaliyopatikana kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa upande wakinamama.
Na katika baadhi ya nchikama China, Urusi,
Vietnam na Bulgaria siku hii ni mapumziko ya kitaifa na hii yote ni katika
juhudi za kutambua mchango wa wakinamama katika kuleta mabadiliko katika jamii.
Ni katika kuadhimisha siku hii muhimu
wanawake wote duniani huja pamoja na kutafakari jinsi ya kuendelea kumuelimisha
mwanamke na kama usemi maarufu usemao, ukimwelimisha mwanamke ni sawa na
kuelimisha jamii nzima.
Hapa nyumbani kwa miaka ya hivi karibuni
wanawake wamekuwa wajasirimali wazuri na wenye msaada mkubwa katika familia
(kaya) na taifa kwa ujumla.
Siku ya Jumatatu mwezi Julai, mwaka jana,
Tigo Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Cherie Blair kwa ajili ya wanawake
(CBFW), USAID na FINCA walizindua mpango mkakati wa wanawake wajasiriamali.
Hiyo yote ni kuonyesha ni kwa vipi kampuni
hiyo yaTigo Tanzania inavyothamini jamii kwa kuweza kurudisha sehemu ya mapato
yake kwa wananchi kupitia kitengo chake cha Huduma kwa Jamii (CR) ili
kumwezesha mwananchi wa kawaida na hasa mwanamke mwenye kipato cha chini.
Mpango huo unajulikana kama Wezesha
Wanawake kwa Maendeleo, umelenga kuwapa uwezo wanawake zaidi ya 3,200 ambao ni
mawakala wa Tigo pesa nchini, kwa kuwapa elimu ya kutunza fedha na kupata
masoko katika biashara zao.
Wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa
Tigo, Diego Gutierrez alisema lengo la mpango huo ni kuwapatia fursa wanawake
mawakala wa Tigopesa.
“Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa,
wanawake wanamiliki karibu asilimia 70 ya uchumi wa Afrika, kwa hiyo Tigo
inajisikia fahari na heshima kushirikiana na Taasisi ya Cherie Blair, USAID na
FINCA katika kutengeneza mazingira ambayo yatawahakikishia wanawake nafasi ya
kupata misaada ya kifedha, masoko, mafunzo na mawasiliano ya teknolojia,”
“kwa ushirikiano wetu huu na wenzetu
tutaweza kubuni miradi mingi kwa wanawake wa Tanzania pia kuwaongezea fursa za
kupata fedha na masoko,” anasema Gutierrez tangu uzinduzi mpaka sasa Tigo imekuwa
ikiwapa wajasiriamali hawa mafunzo kuhusu mbinu za kupata mikopo na usimamizi
wa biashara ili kuwajengea uwezo wa kusimamia miradi yao kwa maslahi ya kwao na
taifa kwa ujumla.
Kwa upande wakinamama wajasirimali, Happy
Mabeba, anasema mpango mkakati wa Tigo Tanzania ni faraja kubwa kwa wanawake
nchini kwa sababu imemuondoa katika dimbwi la umasikini na utegemezi kwenye
familia yake.
Mabeba anasisitiza kwamba kampuni ya Tigo
Tanzania na mpango wao wa Wezesha Wanawake kwa Maendeleo ni fursa pekee kwa
wanawake nchini ambao tatizo lao kubwa ni mitaji ya kuanzisha biashara
mbalimbali.
“Kila mwanamke angependa kuwa na maisha ya
kumfanya kuishi bila kutegemea zaidi kwa mwanaume, tumepokea vizuri mpango ule
wa Tigo na tunatunaendelea kusogea kutoka tuipokuwa hadi sehemu nyingine nzuri
zaidi,”
Na Rose Rwejuna (33) anasema kwamba baada
ya Tigo kuanzisha mpango mkakati wa kusaidia wakinamama kupitia bidhaa yake ya
Tigopesa maisha ya wakinamama na wasichana wengi yamebadilika kwa kiasi
kikubwa.
“baada ya kufungua kibanda changu cha
Tigopesa sasa ninaweza kusomesha watoto wangu na kutunza familia bila matatizo
yoyote , natoa shukurani za kipekee kwa Tigo,” anasema
Anasema kwamba kwa muda mrefu alikuwa hana
kazi ya kufanya wala kipato cha kuweza kujitunza na kutunza familia yake lakini
baada ya kampuni ya simu ya Tigo kuanza kusaidia wakinamama amepiga hatua kubwa
sana kimaisha.
Zulfa Omari ambaye anamiliki kibanda cha
Tigo pesa maeneo ya manzese tip top,
anasema kwamba alipata mkopo kutoka Tigo Tanzania wa fedha taslimu
shilingi 300,000 na kuanza rasmi kazi
yake ya uwakala mwaka jana mwezi wa Oktoba na inakwenda vizuri.
“kwa kweli napenda nachukua fursa hii
adhimu kuwashukuru viongozi wote wa kampuni ya simu ya Tigo kwa msaada wao kwa
sababu kwa sasa naweza hata kusomesha watoto wangu wawili mmoja sekondari na
mwingine shule ya msingi,” alisema.
Kwa upande wake Dannis Minga yeye ni
wakala wa Tigo pesa maeneo ya Ubungo maziwa anasema kwamba alipata mkopo
kupitia Tigo wa shilingi 300,000 na kwa sasa ana mtaji wa shilingi milioni moja
na lakin tano (1.5m) na ameweza kufungua biashara nyingine ya vipodozi ambayo
inamwingizia kipato kwa ajili ya familia.
“yaani sijui nisemeje! Tigo wamekuwa
msaada mkubwa sana katika maisha yangu binafsi kwa kunitoa kutoa sehemu moja
kwenda nyingine na mshukuru Mungu mwanangu anasoma bila matatizo shule ya
msingi sasa,” aliongeza
Katika kuadhimisha siku ya wanawake
Jumamosi ya kesho kampuni hiyo ya Tigo Tanzania watagawa zawadi mbalimbali kama
mabegi, vocha za bure, T-shirts na peni katika baadhi ya maduka yake kama vile Mlimani
city, Tegeta (Kibo Complex), Quality Mbagala shop, Kigamboni, Mbeya, Tanga na
duka jipya Mtwara.
Mwisho.
Post a Comment