Muungano wa Tanzania ni kielelezo cha umoja na maendeleo
Na Jovina Bujulu
Muungano wa Tanzania umeendelea kuwa nyenzo na
utambulisho muhimu katika kuleta umoja na maendeleo katika taifa.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano) Mh. Samia Suluhu Hassan wakati wa mkutano na waandishi wa
habari leo mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais( Muungano) Samia Suluhu Hassan akiongea na waandishi wa habari( Hawapo Pichani) kuhusu mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika utekelezaji wa masuala ya Muungano wakati wa Mkutano leo Mjini Dodoma. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Ofisi hiyo Bi. Siglinda Chipungaupi. |
“Miaka 50 ya Muungano imekuwa ni ya mafanikio
makubwa ambayo yamewanufaisha wananchi katika nyaja mbalimbali kijamii,
kiuchumi, na Kisiasa” amesema Waziri Suluhu.
Waziri Samia amesema kuwa muungano huo umeendelea
kuwa kielelezo imara katika suala la ulinzi na usalama hali iliyowezesha kuwepo
kwa amani na utulivu nchini.
Katika suala la haki za binadamu Waziri Samia amesema
kuwa suala hilo limeendelea kupewa kipaumbele ndani ya katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ambapo wananchi wameendelea kupata haki zao za msingi
kupitia mahakama za Mwanzo hadi za Juu.
Akifafanua kuhusu suala la elimu Waziri Samia
alibainisha kuwa wanafunzi wenye sifa Tanzania Bara na Zanzibar wanapatiwa
mikopo ili kukidhi gharama za Masomo, hali iliyosabisha uimarishwaji wa elimu
ya juu kwani kuwekuwepo kwa ongezeko la vyuo vya elimu ya juu kutoka 25 mwaka
2015 hadi 63 vilivyopo sasa.
Aidha Waziri Samia amesema kuwa Serikali hizi mbili
zinashirikiana katika kubuni na kuibua miradi ya Maendeleo inayofadhiliwa na
Serikali kwa Kushirikiana na Wahisanai wa Maendeleo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais( Muungano) Samia Suluhu Hassan leo mjini Dodoma. |
“Serikali hizi zimekuwa na ushirikiano wa pamoja
katika masuala ya mandeleo mfano Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF III, MACEMP,
ASDPL na ASDP kwa ujumla imekuwa ni chachu kubwa ya Maendeleo ya wananchi katika
pande zote za Muungano” Amesema Waziri Samia.
Waziri Samia aliongeza kuwa Maadhimisho ya Miaka 50
ya Muungano yalizinduliwa Zanzibar tarehe 1 Machi na Rais wa Zanzibar Dkt. Ally
Mohamed Shein ambapo nembo ya Muungano ilizinduliwa na sherehe za Muungano
zitafanyika Dar es Salaam.
Kauli mbiu ya Mwaka huu ni “Utanzania wetu ni
Muungano wetu, Tuulinde, Tuumarishe na Kuudumisha.”
Mwisho
Post a Comment