Msongamano
wa magari jijini Dar es Salaam unaweza kusimuliwa kwa namna nyingi.Ukweli ni
kuwa, kila anayeishi jijini hapa ana maelezo yake kuhusu anavyoathirika namsongamano
wa magari. Maeneo sugu ya foleni ni yale ya makutano ya barabara kubwa na sehemu
nyingine ni zile ambazo huathirika wakati mvua zikinyesha. Hivi karibuni Rais Jakaya
Kikwete alieleza kuwa katika kipindi chake cha pili atahakikisha jiji la Dar es
Salaam linapata barabara za juu maarufu kama ‘fly-over’.
Kwa
mujibu wa Rais Kikwete, barabara hizo zitajengwa katika maeneo ambayo
yanakutanisha barabara mbalimbali na maeneo yanayokabiliwa na msongamano mkubwa.
Barabara zinazopewa kipaumbele katika ujenzi wa flyovers ni zile za Mwalimu Nyerere
na Morogoro. Lakini hizi bado ni kauli tu ambazo hazijaanza utekelezaji hali inayofanya
kuendelea kumomonyoka kwa uchumi wa taifa na wa mtu mmoja mmoja. Ni jambo la
wazi kuwa idadi ya magari inaongezeka kwa kasi jijini hapa, hali hii inaonesha kwamba
watu kumiliki magari sio tena kitu cha anasa bali inatokana na uduni wa usafiri
wa umma.
ATHARI
ZITOKANAZO NA MSONGAMANO WA MAGARI
Wachangiaji
wa mjadala huu wamebainisha athari zitokanazo na tatizo la msongamano wa magari
katika jiji la Dar es Salaam. Zipo athari nyingi za kiuchumi, kijamii na
kimazingira. Imebainishwa kwamba misongamano ya magari inachangia kwa kiasi
kikubwa kuporomosha uchumi wa watu binafsi wa taifa na hata kuendeleza umaskini
(Dk. Khamis).
Wananchi wanalazimika kutumia kiasi kikubwa cha mafuta (pesa) kutembea mwendo mfupi. “Angalia muda unaopotea barabarani na petroli/dizeli na mafuta mengine ya kulainisha mitambo inayopotea bure hasa ukizingatia kwamba vyote hivi tunaagiza nje ya nchi” ni hifadhi ya fedha za kigeni kiasi gani benki kuu inatumia kununulia bidhaa hizi,” alihoji Festo Maro. Vile vile athari zingine zilizoainishwa ni pamoja na uharibifu wa mazingira kutokana na hewa mkaa inayotolewa na magari yanayotumia muda mrefu njiani yakiwa yananguruma bila
kutembea.
Vile vile watumiaji wa magari hayo hufika katika sehemu zao za kazi na hata majumbani
mwao wakiwa wamechoka na hivyo kutokufanya shughuli zao ipasavyo.
Moja ya Barabara za juu almaarufu kama 'Fly Overs" |
Ujenzi wa Dar
es Salaam mpya
Wachangiaji
wengi katika mada hii wanakubaliana na hoja ya ujenzi wa mji mwingine nje ya Dar
es Salaam na kuacha mji wa zamani kama ulivyo ili kuhifadhi historia yake kwa
vizazi vijavyo. Dk Omari Khamis anasema;”Mji huu mpya ujengwe kwa makini sana
ili tuepuke msongamano si wa magari tu bali hata wa nyumba. Ofisi za serikali zisambazwe
na kila eneo liwe na huduma zote za kijamii zinazohitajika katika maisha ya kila
siku kwa mfano maduka, hospitali, vituo vya polisi, shule na mahoteli n.k”
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Ujenzi Bw. Mrtin Ntemo |
Magari ya mradi wa mwendo kasi |
Foleni katikati ya jiji, makutano ya Askari monument mauungio ya Barabara maarufu ya Samora jijini Dar Es Salaam. |
Post a Comment