Mabingwa wa Uingereza, timu ya Manchester United imekuwa timu ya pili na ya mwisho kutoka Uingereza kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya mashindano makubwa ya vilabu barani ulaya mara baada ya kuifunga mabingwa wa ligi ya Ugiriki timu ya Olmpiakos kwa jumla ya mabao 3-0
Mchezaji Robin Van Persie ndiye aliyekuwa shujaa wa mchezo huo mara baada ya kuifungia timu yake hiyo mabao yote matatu maaraufu kama Hat trick na kuifanya timu ya Manchester United kuungana na timu nyingine ya chelsea toka Uingereza mara baada ya wawakilishi wengine waili timu ya Arsenal na Manchester City kuishia kwenye hatua ya timu kumi na sita bora.
Kwa kufanya hivyo timu ya Manchester imeweza kuvunja rekodi yake iliyoiweka tarkibani miaka 19 iliyopita mara baada ya kuwatoa Barcleona mnamo mwaka 1995 kbaada ya kuwa imefungwa nmabao 2-0 katika mchezo wa awali na Robin Van Persie kuwa mchezaji wa kwanza wa United kuifungia timu yake mabao matatu.
Kocha mkuu wa timu hiyo ambaye yuko kwenye wakati mgumu kutokana na mwenendo wa Mabingwa wao msimu, David Moyes alinukuliwa akisema ni wachezaji wachache sana duniani wanaoweza kufanya mambo aliyoyafanya Robin Van Persie na hivyo kumshukuru sana na kusema hakika ni mmoja kati ya wachezaji bora kabisa duniani kutokana na kiwango alichoonyesha jana usiku katika mchezo huo wa marudiano.
Mfungaji wa mabao matatu ya Manchester united katika mchezo wa jana, Robin Van Persie |
Robin Van Persie na Wayne Rooney wakishangilia bao la tatu walilokuwa wameshirikiana kujipanga katika upigaji wa faulo ndgo langonimwa Ol yalioungwa na Van Persie katika mchezo wa jana. |
Post a Comment