Kuna uwezekano wa ndege ilipotea ya shirika la ndege la Malysia kuwa imezama katika bahari ya india .
Kupotea kwa ndege hiyo yenye nambari
MH370 kuna uwezakno ya kuwa umesababishwa na kushindwa kufanya kazi kwa ghafla kwa moja ya
mifumo ya kundeshea ndege hiyo kama ilivyotanabaishwa leo hii asubuhi na
bosi wa shirika hilo.
Ofisa mkuu wa shirika hilo bwana
Ahmad Jauhari Yahya amesema ya kuwa wataalamu wa ajali hiyo wanaendelea kufanya
utafiti endapo kugudungua kama kuna uwezazakno wa kufanana na tukio la ndege
nyingine ya shirika hilo ya aina ya Boeing 777 iliyotokea mnamo mwaka 2005.
Ndugu wa wahanga wakiwa wanatokwa na majonzi |
Katika tukio hilo ambalo lilitokea wakati ndege hiyo ilipokuwa ikitaka kuruka tokea mjini Perth, Australia kwenda Kuala Lumpur na mara ghafla baada ya kuwa inapaa ikatokea hali ya isiyokuwa ya kawaida ghafla kwa kuruka juu kwa kasi na kukaribia kuzima kabisa katika chumba cha kuendeshea ndege hiyo na kulazimu mmoja wa wahudumu wa ndege hiyo kuanza kusali na mwingine aliyekuwa ameshikilia trei la vinywaji kulidoshosha chini kabla ya rubani wa ndege hiyo kufanikiwa kuokoa ndege hiyo.
Mfano wa ndege ya shirika kama ambayo haijulikani ilipo mpaka sasa |
Mawasiliano ya ndege hiyo MH370
yalizimika ghafla mara baada ya kupaa kwa ndege hiyo mnamo tarehe 8, mwezi huu
na kuna uwezekano ikawa ilisababishwa na moja ya mifumo ya kuendeshea a ndege
hiyo kushindwa kufanya kazi tofauti na inavyodhaniwa huenda kuna mtu alifanya
hivyo.
Mwenendo wa ndege hiyo kwenda usawa wa
magharibi unaweza ukawa ulisababishwa na rubani wa ndege hiyo katika jitihada
za kutaka kuepusha na ajali hiyo, aliendelea kusema bosi huyo na kusema ,"
Kwa kweli hatujui ni kwa nini na hatutaweza kujua mpaka pale waokoaji
watakapofanikiwa kukipata kisanduku cheusi cha kurekodia matukio yanayotokea
kwenye ndege.
Moja wa picha za Satelite ya mwenendo wa ndege hiyo katika upande wa mashariki mwa bahari ya India |
Ndugu wa wahanga wa ajali ya ndege wakitaka majibu nje ya ofisi za ubalozi wa Malaysia nchini China |
Ndugu wa wahanga wa ndege hiyo wakiandamana nje ya ubalozi wa Malaysia nchini China leo asubuhi |
Post a Comment