Makangale SATELLITE Tanzania hivi karibuni ilifanya mahojiano na Mjasiriamali na mbunifu wa mavazi nchini Doreen Noni aliyehudhuria mkutano wa uchumi duniani uliofanyika huko Davos, Uswisi mwezi uliopita juu ya yote anazungumzia nafasi ya wanawake, vijana na ujasiriamali endelea…….

Makangale SATELLITE: Tafadhari hebu jitambulishe wewe ni nani?

Doreen: kwa jina mimi naitwa Doreen Esthezia Peter Noni 
Doreen Noni
Mwanadada mjasiriamali, Doreen Noni
Makangale SATELLITE : umezaliwa wapi?

Doreen: Nimezaliwa Dar es Salaam, mwaka 1989 mwezi wa tatu, tarehe 10 na nina kaka zangu wawili , mimi ni mtoto wa tatu na mwisho kuzaliwa  na wa kike pekee na wazazi wangu pia ni wajasiriamali 

Makangale SATELLITE: Ulisoma wapi?

Doreen: Nilisoma Upanga Nursery School na baada ya hapo nikahamia Nairobi kuanzia darasa la sita mpaka form six nilikuwa Brook High School, Nairobi 

 Makangale SATELLITE: Je chuo ulisoma wapi?

Doreen: chuo nilisomea Uingereza, Nottingham Trent University na nilisomea mambo ya Multi aMedia 

Makangale SATELLITE: Ulipata nafasi ya kuhudhuria mkutano wa uchumi duniani hebu tueleze ulipata vipi nafasi ya kuhudhuria?

Doreen:  Mimi nilipata nafasi ya kuhudhuria (World Economic Forum) kupitia asasi ya Global Shapers ambayo ni delegation ya vijana kupitia World Economic Forum na vijana kuanzia  miaka 20 mpaka 30 ambao kazi yao kuu ni kuangalia vijana ambao wanaleta  mabadiliko katika jamii na ushiriki wa vijana katika maeneo mbalimbali, ya ujasiriamali kwa hiyo nilituma maombi kwenye jukwaa la Uchumi Duniani na wao wakaona nafaa kuhudhuria na nikahudhuria kwa hiyo nikawa mjumbe wa World Economic Forum kama kijana na jukwaa la kuwakilisha vijana wa bara la Afrika na nimehudhuria mikutano mitatu ya uchumi duniani.

Makangale SATELLITE: Je kwenye mkutano huu wa hivi karibuni nini kilijitokeza? 

Doreen:  nilikuwa kwenye session tofauti nilikuwa kwenye panelist mbalimbali, kama vile Innovation and design na panelist nyingine ilikuwa Africa the next billionaire ambayo kulikuwa na marais mbalimbali kama vile Goodluck Ebele Jonathan; Rais wa Nigeria, Aliko Dangote; Afisa Mtendaji Mkuu wa Dangote Group na John Mahama; Rais wa Ghana, hii session ilikuwa inaogelea kuhusu umati wa watu Afrika na vijana tulikuwa kama 50 ambao tulihudhuria mkutano huu na vijana wengi Afrika wanatuma maombi duniani na kila session wanataka vijana wahudhurie kwa hiyo wanataka kujua uwezo wa vijana katika maswala mbalimbali ya kiuchumi, kijamii na kijamii.

Makangale SATELLITE: je unafikiri nafasi ya Tanzania kwenye mkutano kama huu ikoje?

Doreen: yaani kwa kweli ukiniuliza Tanzania kama nchi kwa kweli ni ngumu kwa sababu mimi sijakaa sana nchini na kwa sasa najifunza kuhusu nchi yetu lakini kwangu kwa kipindi kirefu sikuwepo hapa nyumbani. Lakini kwa vijana mikutano hii ni mizuri kwa kujifunza  

Makangale SATELLITE:  ulianza lini kazi yako ya ubunifu?

Doreen: nilianza 2011 na kusajili kampuni yangu mwaka huo huo na inaitwa Miracle films and Studio, tuna shoot kazi mbalimbali films, matangazo na nilianza rasmi swala la ubunifu wa nguo mwezi wa Machi mwaka huo huo nikaanza taratibu na watu wakawa wananipa mrejeo (feedback) nzuri na (positive results) na ndiyo zimenifanya niendelee na kazi hii ya ubunifu wa mavazi

Makangale SATELLITE; Changamoto ngani umekutana nazo kwenye kazi yako hii ya film na ubunifu wa mavazi?

Doreen: changamoto kama kijana self discipline, na kupata mawazo, cha pili ni mental ship kama kuna watu wa kukupa mawazo ni vema na timu ya kufanya nayo kazi lakini mindset ya watu ni kupata pesa tu lakini mimi nataka kutengeneza empire kwa hiyo ni muhimu kupata timu bora ya kufanya nayo kazi. 

Makangale SATELLITE: Ni kitu ngani unapenda na nini hupendi?

Doreen: Sipendi uongo kabisa, wote ni watu wazima, mimi ninachopenda ni ukweli, kudanganya kunaleta matatizo mengi. Uaminifu ni muhimu inatuwezesha kuokoa muda kwa sababu ya ukweli, muda ni muhimu sana kwa maisha ya binadamu kwahiyo sipendi uongo kabisa, na kwa kupenda napenda wazazi wangu na marafiki zangu tu

Makangale SATELLITE: umeolewa?

Doreen: Single
Makangale SATELLITE: Nini siri ya mafanikio yako?

Doreen: Mindset (Mtazamo)

Makangale SATELLITE: Ukiwa mapumziko unafanya nini?
Doreen: napenda kusafiri kuongea na kukutana na watu tofauti lakini pia napenda kufanya mazoezi 

Makangale SATELLITE: Je watu wanaokuzunguka wanasemaje kuhusu wewe?

Doreen: wana heshimu kazi yangu na kunitia moyo kwa kila kitu ninachofanya

Makangale SATELLITE: unazungumziaje hali ya wanawake hapa nchini na ushauri wako kwao?

Doreen: wanawake wajasiriamali wawe wanafanya kazi kwa bidii lakini ni lazima wajitambue na malengo yao ya baadaye na kujipanga kwa ajili ya maisha yao.

Mwisho  
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.