WASWAHILI huwa wana msemo wao ," Kila Chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho," hakika haya ni maneno yenye kutoa kila aina ya kiashiriao ya kwamba kila jambo lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho, ukianzia katika siasa, burudani wote ni mashahuda kwa  jinsi tulivyoona mwisho wa kundi maarufu la muziki wa roki la Uingereza lilijulikana kama,"TheBeatles" lilivyotamba kwenye miaka ya sitini na sabini lakini leo liko wapi, tumeshuhudia pia wanasasiasa maarufu  kama wa kina Joseph Desire Mobutu Sese Seko, Muamar Ghadafi wa Libya, na kina Michael Jakson aliyekuwa mfalme wa mziki wa Pop duniani ila leo hii wako wapi wote hawa.


Hata kwenye soka au kandanda wote tuliona miaka ya themanini na tisini kwa jinsi nchi ya  Brazili ilivyotawala kwenye kandanda la Dunia ikiongozwa kuanzia na kizazi cha kina Pele, Garincha, Bebeto, Romario na mwisho Ronaldo ila  leo wako wapi na sasa tunaona jinsi waliokuwa wabaitwa wafalme wa  kandanda kwenye ngazi za vilabu Duniani,  timu ya Barcelona ya Uhispania walivyopotea jana usiku ikiwa ni vipigo mfufulizo katika michezo ya kuwania vikombe mara baada ya kuchapwa pia mabao 2-0 na timu ya Ac Milan katika mpambano wa raudni ya kwanza ya mchezo wa Klabu Bingwa ya Ulaya al maarufu kama EUFA Champions lLeague, na kufuatika jana kutolewa kwenye kombe la mfalme , Copa De Relay kwa jumla ya mbao 4-2 na timu hasimu wake Real Madrid hii inadhirhirisha kabisa ya kwamba sasa mwisho wa kutawala umefikia mwisho kwani timu kama Real MAdrid au Ac Milani hakuna ambye ajuye ya kwamba zimeundwa upya kwa damu changa.
Mfalmwe wa Zaire, King Joseph Desire Mobutu Sese Seko


Jana tumeshuhudia jinsi mwanasoka bora wa Dunia kwa mara nne mfufulizo, Lionel Messi alivyokuwa anataabika uwanjani , vile vile tumemshuhudia Nguli na nahodha wa klabu hiyo Calos Puyol akiudhihirisha ulimwengu ya kuwa umri una mantiki kubwa kwenye soka kwa jinsi alivyokuwa anatamani kucheza lakini mwili unakataa, hayo ni badhi tuu ya matukio ambayo yanatoa mwelekeo ya kuwa sas mwisho wa Barcelona umewadia.

Barcelona kama ilivyokuw imezoeleka ni timu yenye kutandaza mpira safi na kutafuta vyumba vya kufunga ila jana usiku hali ilikuwa tofauti kabisa si barcelon tuliyokuwa tumezoea ikiitesa Real Madrid nyumbani na ugenini, wote tulishuhudia hata fundi wao Xavi alivyokosa ufundi na mwisho wake kuishia kutolewa na kuingizwa damu mpya ya Thiago Alcantara (21) kusema ukweli kizazi hiki kimefikia tamati.

Ukianzia Golikipa Jose Manuel Pinto mwenye miaka 37, Calos Puyol 34, Andre Iniesta 28, Xavi Hernandez 33, David Villa 31, Dani Alves 29 ni dhahidi kabisa ya kuwa sasa kizazi hiki cha dhahabu kimefikia tamati na kutuokana na kubadilisha mara kwa mara wachezaji imechukua muda kuweza kuingiza Damu changa kama Thiago Alcantara (21), Busquets (24), Jordi Alba (23) au Sergio Gomez(20) mapema kuweza kuendana na mfumo wao.

Cristiano Ronaldo and Sergio Ramos
Mfalme mmoja anazama mwingine mwingine anaibuka


Cristiano Ronaldo and Jose Pinto
Kipa namba mbili wa Barcelona, Jose Maria Pinto akijaribu kuzuia mchomo wa kiki ya penati ya Cristiano Ronaldo pasipo mafanikio.

Jordi Alba
Mchezaji na beki wa Barcelona, Jordi Alba akishangilia goli la kufutia machozi na kufanya matokea kusomeka 3-1



Real Madrid
Wachezaji wa Real Madrid wakiwapungia mashabiki wao mara baada ya kuiondoa timu ya Barcelona kwenye mashindano ya kombe la mfalme, Copa De Leray.

Carlos Puyol and Lionel Messi

Wafalmwe wa Nou Camp, Nahodha Calos Puyol na Lionel Messi wakitoka uwanjani vichwa chini pasipo kuamini yakiyotokea kwa kukubali kipicho cha mabao 3-1 toka kwa mahasimu wao Real Madrid.

























































































Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.