Timu ya Yanga ya mjini Dar es Salaam jana ilifanikiwa kuidimiza timu ya Azam pia ya jijini Dar es Salaam kwa bao moja kwa bila 1-0 katika muendelezo wa michezo ya Ligi kuu ya Tanzania al maarufu kama Vodacom Premier League. Bao la liliwapatia ushindi huo murua vijana hao wa mitaa ya Twiga na Jangwani lilifungwa na mchezaji wa Kimataifa kutokea Nchnini Rwanda,?Haruna Niyonzima.
Wakati hayo yakiajiri kwa upande wa Tanzania, Nchini Uingereza ligi kuu ya nchi nayo iliendeleza kupamba moto wakati Mabingwa wa kihistoria katika nchi timu ya Manchester United iliendelea kupaa kileleni mwa msimamo waligi hiyo ikiifunga timu inayoshika mkia timu ya Queen Park Rangers kwa mabo 2-0. Mabao ya timu hiyo yalitiwa kimiani na mchezaji anayekuja kwa kasi kutoka nchini Brazili Beki Raphael Da Silva na goli lingine lifungwa na mkongwe wa timu hiyo Ryan Giggs.
katika micehzo mingine ya ligi hiyo timu ambayo kocha wake kwa sasa yuko katika kipindi , timu ya Arsenal ilifanikiwa kupata ushindi kwa mabao 2-1 katika dakika za lala salama kwa magoli yaliofungwa na mchezaji toka Uhispania, Santi Carzola.
wakati hayo yakitokea katika uwanja wa Emirates timu ya Fulham iliidimiza pia timu ya Stoke City kwa goli lililofungwa na mchezaji toka nchini Bulgaria Dimitar Berbatov., nayo Norwich City ikiichambua timu machachari ya Everton kwa mabao ya Grant Holt na Kei Kamara.
wakati hayo yakitokea katika uwanja wa Emirates timu ya Fulham iliidimiza pia timu ya Stoke City kwa goli lililofungwa na mchezaji toka nchini Bulgaria Dimitar Berbatov., nayo Norwich City ikiichambua timu machachari ya Everton kwa mabao ya Grant Holt na Kei Kamara.
Nayo timu inayopigana vita ya kutokushuka daraja ya wigani ikaifunga timu ya Reading kwa jumla ya mabao 3-0
Mchezaji wa Yanga, Jerry Tegete akijilaumu mwenyewe mara baada ya kukosa goli la wazi |
Moja ya Vituko vilionekana jana katika mchezo wa Yanga na Azam zote za jijini Dar es Salaam. |
Santi Carzola akishangilia moja ya mabao yake aliyoyafunga jana dhid ya Aston Villa
Mchezaji wa Arsenal Santi Crzola kipatia timu yake goli la ushinid dhidi ya Aston Villa katiak ushindi wa 2-1
Mchezaji toka Bulgaria Dimitar Berbatov akiifungia timu yake ya Fulham goli la pekee na la ushidi katika mchezo wao wa jana dhidi ya Stoke City.
Moja ya purukushani ya zilitokea golini mwa Fulham,hapa ni mmoja wa wachezaji warefu katika ligi hiyo Peter Croch akijaribu kumzidi maarifa beki wa timu ya Fulham.
Mchezaji Grant Holt akishangilia mara baada ya kufunga goli la ushindi dhidi ya timu ya Everton katika ushindi wa 2-1
Mchezaji anayeichezea Norwich kwa mkopo akitokea Sporting Kansas City ya Major League, Kei Kamara akishangilia moja ya mabo ya Norwich katika mchezo huo wa jana.
Mchezaji machachari toka Brazil, Raphael Da Silva akiipatia timu yake ya Manchester United goli la kuongoza dhidi ya Queen Park Rangers.
Mkongwe Ryan Gigg akiiandikia timu yake ya Manchester goli la pili na ushindi dhidi ya timu iliyo mkiani ya QPR
Mchezaji toka Ivory Cost, Arouna Kone akishangilia moja ya mabao aliyofunga jana katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Reading
Mchezaji Rumelo Lukaku akishangilia moja ya mabao ya West Brom katika ushindi wa 2-1 dhidi ya timu ya Sunderland
Mchezaji toka Nigeria, Peter Odemwinge akifurahi kurudi katika mchezo dhidi ya Sunderland itakumbukwa mchezaji huyo alikuwa amefungiwa kucheza baadhi ya michezo katika kile kilichoshutumiwa kama utovu wa ndihamu katika kulazimisha kuhama timu hiyo kwenda Queen Park Rangers katika dirisha la January.
Post a Comment