Picture
Hali ilivyo katika hospitali ya Mwalimu Nyerere, Butiama, Mara
HALI ya hospitali ya Butiama iliyopo wilayani Musoma mkoani Mare, iliyofunguliwa rasmi mwaka 1972 na marehemu Mwalimu Julius Nyerere imezidiwa na wagonjwa kutokana na kuachwa kama ilivyoziduliwa enzi za Mwalimu.

Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dk Joseph Musagasa, alisema kuwa hali hiyo imekuwa kama kawaida kwa sasa ambapo inafikia hatua wagonjwa wanapokuwa wengi kitanda kimoja wanalazimika kulazwa watoto wanne.

“Kitanda kimoja wanalazwa watoto wanne na hii hali mliyoikuta leo ya watoto wawili wawili kwenye kitanda kimoja ni nafuu,’’ alisema Dk Musagasa.

Alisema kuwa mbali na wodi ya watoto, mpaka sasa kuna vitanda nane tu vya wagonjwa wa kiume ambapo vikijaa vitanda hivyo wagonjwa wengine hulazimika kulazwa sakafuni na kwamba umefika wakati hospitali hiyo inatakiwa kufanyiwa upanuzi wa majengo haraka na vifaa vikiwemo vitanda.

Soma habari nzima kwenye: Kalulunga blog
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.