Inastajajabisha lakini huu ndio ukweli wenyewe mwanafunzi wa miaka tisa (9) wa darasa la pili  jina kapuni kutoka shule ya msingi ya bunge mjini Dar es Salaam jana alifikishwa katiak vyombo vya dola akiwa anatuhumiwa kumwimbia mwalimu wake.

Mwalimu huyo aliielezea ya kwamba mwanafunzi huyo alifika katika ofisi za walimu na kudai ya kwamba mwalimu wake kamtuma amchuhulie begi lale la mkononi Almaarufu kama " Handbage" na mara baada ya kukabidhiwa handabage hiyo mwanafunzi huyo alitokomea nalo mahali pasipokujulikana hadi pale mwalimu wake alipochukua hatua za kumfuatilia na kumfikisha katika vyombo vya dola kwa msaada zaidi wa kupatikana kwa mali zake zilizokuwemo ndani ya handbage hiyo.

Katika kuhojiwa mtoto huyo alidai ya kwamba begi alililichukua na fedha taslimu shilingi laki mbili na elfu themanini na tano (285,000/=) zilizokuwemo ndani ya pochi ndogo ndani ya handbage hiyo alizichukua  na kuzitumia na wenzake na kuhusu vyeti vilivyokuwemo ndani ya handbage hiyo na stakabadhi nyinginezo alizichana na kuzitupa kwenye mfereji na hadi tulipokuwa tunakwenda mtamboni kijana huyo aliendelea kuhojiwa kwa kina ili kujua wapi handabage kubwa lilipo kwa kuwa kulikuwa na vitu vingine kama vile simu na nyaraka nyingine za dhamani.

Mzazi wa kijana huyo alikuwemo pia katika kusaidia kuhusu upotevu huuo na kulingana na umri wa mwanawe ili kusaidia katika kupatikana kwa mali hizo za mwalimu wa mwanawe.


Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.