Roberto Manchini, kocha wa Manchester City jana alihidhiisha ya kuwa yeye ni bora zaidi ya Rafael Beitez mara baada ya kuiongoza timu yake kutoka na ushindi mnono wa mabo 2-0 dhidi ya timu ya Chelsea.
Alikuwa ni mchezaji bora wa Africa, Yaya Toure ambaye alipata mpira katika eneo la hatari katika dakika ya 63 na kuwapiga chenga mabeki kama watatu hivi na kumchungulia kipa Peter Czech alivyokaa na kuupeleka mpira upande wa kushoto na kumwacha akigaa chini pasipo mafanikio kabala ya Carlos Tevez kumalizia msumari wa mwisho katika dakika ya 85.
Nayo timu ya Swansea jana ili endelea kujiandikia historia mpya ikiwa kama timu ya kwanza toka Wales kushirikia ligi kuu ya Uingereza, Premier League jana ilienda mbali zaidi ikijiandikia historia nyingine kwa kuwa timu ya kwanza kunyakua kombe la Ligi baada ya kuinyanyasa vilivyo timu ya daraja la pili ya Bradford City. Itakumbukwa Bradford ilifanikiwa kucheza fainali za kombe hilo mara baada ya kuviondosha timu vigogo vya ligi kuu kama vile Aston Villa, Arsenal na Wigan.
Alikuwa ni winga machachari wa timu hiyo Nathan Dyer na Jonathan De Guzman waliyopeleka kilio Bradford mara kila moja wao kufunga mabao mawili katika mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa Wembely na mchezaji mwenye uchu wa kufunga Michu kumalizia msumari wa magoli na kuisasambua timu hiyo kwa jumla ya magoli 5-0 na kuhudhuiriwa na watazamaji wapatao takrinbani 82,597.
Itakumbukwa Swansea haijawi kunyanyua kombe lolote lile kwa takribani ya miaka 101 na hiyo itakuwa ni furaha na historia kubwa kwao kwani mara baada ya kunyakua kiombe hio pia wamepata nafasi ya kushiriki kombe la Europa msimu ujao.
Dosari kubwa iliyojitokeza ni pale wachezaji Nathan Dyer na Jonathan De Guzman waliponyanganyana mpira kila mmoja akitaka kupiga mkwaju wa penati mara baada ya Jonatha De Guzman kufanyiwa madhambi na Matt Duke na Dyer kutaka kupiga mkwaju huo ili afikishe jumla ya mabao matatu na kufanya afunge hatrick na kuweka historia ya kufunga hatrick katika fainali hizo a kihistoria katika klabu hiyo.

Kipa wa Manchester City , Joe Hart akiruka kuokoa mchomo wa Penati ya Frank Lampard.
Wachezaji Yaya Toure na wakimpongeza kipa wao Joe Hart mara baada ya kuokoa mchomo wa Penati.
Mchezaji Yaya Toure akishangilia kwa furaha mara baada ya kuipatia City goli la kuongoza.
Golikipa wa Chelsea akiwa katika kazi ngumu ya kuokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake.
Joe Hart akimfanyia madhambi mchezaji Demba Ba na kuipatia Chelsea penati lakini hata hivyo Hart alionyesha uhodari kwa kuiapngua penati hiyo iliyopigwa na Frank Lampard.
Post a Comment