BAADA ya kuchapwa Bao 3-1 wakiwa katika uwanja wao waa
Emirates na Bayern Munich kwenye Mechi ya kwanza ya Raundi ya Mtoano ya
Timu 16 ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE (UCL), Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger,
anaelekea kukubali kuwa huu utakuwa Msimu wake wa 8 mfululizo wa ukame
wa Makombe pale aliposema itakuwa vita rahisi kuwania nafasi ya 4 kwenye
English Premier League (EPL), badala ya kutegemea kubaki UCL kwa
kuifunga Bayern huko kwao Allianz Arena katika marudiano.
Mara baada ya Mechi hiyo ya Arsenal na
Bayern Munich kumalizika, Wenger, alionyesha waziwazi kuumizwa na
kipigo na hakupeana mkono na Meneja wa Bayern, Jupp Heynckes, na
Wasaidizi wake na kutimkia moja kwa moja Chumba cha Kubadilishia Jezi
ambako inadaiwa alikaa peke yake kwa Dakika 25.
Kwenye EPL, Arsenal wapo nafasi ya 5
wakiwa Pointi 4 nyuma ya Timu ya 4 Tottenham na hilo lilimfanya Wenger
aibuke toka Chumba cha Kubadilishia Jezi akiamini ni rahisi kuikamata
nafasi hiyo ya 4 na kufuzu kucheza UCL Msimu ujao kuliko kupindua kipigo
cha 3-1 huko Allianz Arena watakaporudiana na Bayern Mwezi Machi.
Post a Comment