Timu ya Nigeria al maarufu kama Super Eagles jana walitangazwa kama mabingwa wapya wa Africa katika mashindano yaliyojulinana kama Orange AFRICON 2013 katika uwanja wa jijini Johannesburg , Africa kusini mara baada ya kuifunga timu ya Taifa ya Burkina Faso kwa bao moja kwa bila (1-0).
Iliwachukua mabingwa hao wa dakika 40 katika kujiandikia historia mpya mara baada ya kujaribu kwa takribani miaka 20 ili kuweza kuwa mabingwa wapya licha ya taifa hilo la Africa magharibi kubarikiwa kutoa moja ya vipaji bora kabisa katika ulimwengu wa kandanda. Alikuwa ni mchezaji Sunday Mba aliwezeza kufunga bao hilo katika moja ya mpira uliopigwa na mshambuliaji Victor Mosses kuwababatiza moja ya mabeki wa Burkina Faso na kumkuta katoka nafasi ambayo aliweza kuuutuliza na kupiga moja kwa moja na kuiandikia Nigeria bao hilo lililuudumu mpaka mwisho wa mchezo.
Kwa ushindi huo unamfanya Stephen Keshi kuwa kocha wa pili katika historia ya mashindano hayo kuchukua ubingwa akiwa kama mchezaji mnamo mwaka 1994 na mwaka 2013 kama kocha mara baada ya Mohamoud Al Gohary kufanya hivyo mwaka 1958.
Mchezaji wa Nigeria na Chelsea ya Uingereza, Vitor Mosses akiwa na wenzake katika kushangilia ushindi
Victoria akinyanyua kombe la ushindi juu kwa furaha na kutabanaisha ya kuwa anafurahia kuwa Mnigeria.
Post a Comment