Katika mchezo wa soka wa kirafiki, timu ya Taifa ya Tanzania imelaza timu ya Taifa ya Cameroon bao moja kwa bila, bao lililofungwa na Mbwana Samatta mnamo dakika ya 89 ya mchezo baada ya kupata pasi ya Erasto Nyoni.

Maelezo ya matukio muhimu wa mechi hiyo kutoka ShaffihDauda.com yanasomeka hapo chini ya picha.

Shukurani ya picha: Yusuf Badi/HabariLeo na Richard Mwaikenda “Kamanda wa Matukio”
Dk 90 FULL TIME! Taifa Stars 1-0 Cameroon.

Dk 89 Goooo..! Mbwana Samatta anaifungia Taifa Stars bao la kuongoza akiunganisha krosi ya Erasto Nyoni.

Dk 85 Cameroon inafanya mabadiliko wametoka Aboubakar Vincent na Bouba wameingia Bakinde Gerard na Makoun Jean.

Dk 83 Amri Kiemba wa Taifa Stars anakosa bao la wazi bao la wazi baada ya mpira aliokuwa akiusubiri kuingiliwa na beki wa Cameroon, Assou Ekotto.

Dk 79 Kaseja anadaka shuti kali la Ashu Clovis wa Cameroon. Walikuwa wamebaki wawili tu.

Dk 73 Cameroon inafanya mabadiliko anatoka Bedimo Henri anaingia Ashu Clovis.

Dk 70 Sure Boy anapiga shuti kali langoni kwa Cameroon lakini beki Ngoula anautoa nje na kuwa kona butu.

Dk 68 Cameroon inafanya mabadiliko anatoka Olinga Fabrice anaingia Edoa Charle.

Dk 66 Sure Boy anapiga shuti kali katika lango la Cameroon lakini kipa Effala Komguep anadaka.

Dk 60 beki wa Cameroon Aminou Bouba anabanwa misuli na kutibiwa uwanjani wakati Taifa Stars ikiwa katika shambulizi kali.

Dk 60 beki wa Cameroon Aminou Bouba anabanwa misuli na kutibiwa uwanjani wakati Taifa Stars ikiwa katika shambulizi kali.

Dk 58 Cameroon inafanya mabadiliko anatoka Tchami Herve anaingia Eloundu.

Dk 56 Taifa Stars inafanya mabadiliko anatoka Mwinyi Kazimoto anaingia Thomas Ulimwengu.

Dk 54 Ngoula wa Cameroon anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Mrisho Ngassa.

Dk 48 Taifa Stars inafanya shambulizi kali langoni kwa Camerooni.

Dk 48 Taifa Stars inafanya shambulizi kali langoni kwa Camerooni.

Dk 45 Kipindi cha pili kimeanza

Dk 45 HALF TIME. Taifa Stars 0-0 Cameroon

Dk 41 Timu zinaendelea kushambuliana kwa zamu na Taifa Stars inafika mara kadhaa langoni kwa Cameroon.

Dk 28 Shomari Kapombe wa Taifa Stars anaonyeshwa kadi ya njano kwa mchezo mbovu.

Dk 26 Taifa Starz inapata penalti ilikuwa krosi ya nyoni kabla ya beki ngoula kushika mpira. Nyoni anapiga anakosa.

Dk 25: Tanzania 0-0 Cameroon

Dk 20 Kipa wa Taifa Stars, Juma Kaseja anatibiwa baada ya kugongana na mshambuliaji mmoja wa Cameroon.

Dk 19 Frank Domayo anaonyeshwa kadi ya njano kwa mchezo usiofaa kwa mchezaji wa Cameroon.

Dk 15 Timu zinashambuliana kwa zamu na zinatawala kwa pamoja sehemu ya kiungo. TAIFA STARS 0-0 CAMEROON
DK 1: Mpira umeanza Tanzania 0-0 Cameroon

LINE UP: TAIFA STAS, Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Kelvin Yondan, Aggrey Morris, Salum Aboubakar 'Sure Boy', Mrisho Ngassa, Frank Domayo, Mbwana Samatta, Mwinyi Kazimoto na Amri Kiemba

Source: http://www.wavuti.com
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.