Miss Ilala 2013, Doris Mollel Ijumaa ya wiki iliyopita alitembelea shule ya msingi Pugu jijini Dar es Salaam na kukabidhi jumla ya vitabu 50 za hadithi kwa wanafunzi wa shule hiyo katika harakati zake binafsi za kuwajengea wanafunzi na watoto utamaduni na tabia ya kujisomea kwenye umri mdogo.
Miss Ilala huyo wa
mwaka 2013 alitumia nafasi hiyo kuwahamasisha wanafunzi kujisomea kama ufunguo
wa maisha yao ya baadaye.
Zifuatavyo ni baadhi
ya picha za tukio hilo wakati wa ukabidhishaji wa vitabu hivyo.
Miss Ilala 2013, Doris
Mollel, akisaini kitabu cha wageni baada ya kutembea shule hiyo ya msingi Pugu
jijini Dar es Salaam.
|
Doris Mollel akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo ya msingi ya Pugu
muda mfupi baada ya kukabidhi vitabu hivyo.
|
Miss Ilala 2013, Doris Mollel akimkabidhi vitabu Mwalimu Josephine
Matiku kwenye hafla rasmi ya makabidhiano shule hapo ijumaa iliyopita jijini
Dar.
|
Miss Ilala 2013, Doris Mollel akipozi na walimu wa shule hiyo wakati wa
halfa ya kukabidhi vitabu.
|
Miss Ilala 2013, Doris Mollel katika picha ya pamoja na baadhi ya
wanafunzi wa shule ya msingi Pugu.
|
Post a Comment