Mfano wa Windows XP |
Baadhi zimeanza kufanyia kazi tatizo hilo, ikiwamo benki moja
ambayo jana alasiri ilituma ujumbe kwa wateja wake kuwa, “Ndugu mteja, kuanzia Jumamosi
saa 2:00 usiku Aprili 5, mpaka Jumapili saa 12:00 asubuhi tutakuwa tunaboresha
mashine zetu za ATM, hivyo kadi yako haitafanya kazi kwa kipindi hiki. Asante.”
Kwa mujibu wa Microsoft asilimia kubwa ya benki katika nchi
zinazoendelea zinatumia programu ya Windows XP katika kuendesha ATM, hivyo kuwa
moja ya waathirika wa mpango huo.
muonekano (interface) ya programu ya windows XP |
Katikati ya Machi, Microsoft ilitangaza kusitisha huduma zote zinazohusiana na bidhaa zake za Windows Xp kufikia Aprili 8, mwaka huu. Pia shirika hilo litasitisha ufanisi wa programu ya kuzuia na kupambana na virusi ya Microsft Security Essentials katika mfumo wa Windows Xp, hivyo kufanya urahisi wa kompyuta zinazoitumia kukosa ulinzi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Twiga Hosting, Jacob Urassa alisema
Watanzania hawatakiwi kupuuza onyo hilo kwa kuwa ikifika Aprili 9 usalama wa
taarifa zao utakuwa hatarini.
“Windows XP ni dhaifu mara tano zaidi ya Windows 7 na 8, kwa
hiyo Microsoft wameona ni bora wakaitoa sokoni. Kwa maana hiyo ATM na kompyuta
zote zinazotumia programu hizo hazitakuwa na ulinzi wa uhakika,” alisema Urassa
ambaye ni mtaalamu wa masuala ya Teknolojia ya Mawasiliano (IT).
Alisema kuwa kuna idadi kubwa sana ya Watanzania wanaoendelea
kutumia bidhaa hizo zikiwemo taasisi kubwa nchini hivyo kuna haja kubwa ya
kuchukua hatua za kubadilika na teknolojia.
Naye, Ofisa Uhusiano wa Benki ya Posta, Noves Moses aliwatoa
wasiwasi wateja wake kuwa licha ya kusitishwa kwa matumizi ya Windows XP, bado
benki hiyo itaendelea kutoa huduma zenye kiwango kile kile.
Post a Comment