Tanzania ni nchi ya nne duniani kwa wagonjwa wa sikosel.
TAASISI ya Sikoseli Tanzania imewaomba wadau wengine wa afya nchini
kujiunga katika mapambano ya ugonjwa wa seli moja yaani sikoseli kwa sababu
utafiti unaonyesha kati ya watoto 8,000 hadi 11,000 kuzaliwa na ugonjwa huo
nchi nzima.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye kampeni ya kuhamasisha
mapambano dhidi ya ugonjwa ambao uliandaliwa na taasisi mbili za Sikoseli
Tanzania na Little Fingers Music mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Makamu
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sikoseli Tanzania, Dkt Julie Makani alisema kwamba
hospitali ya taifa Muhimbili kupokea wagonjwa mia kila wiki ambapo ni asilimia
ishirini tu nchi nzima.
Alisema kwamba ugonjwa huo ni wakurithiwa kutoka kwa wazazi baba na
mama kwenda kwa mtoto na Tanzania ni nchi ya nne duniani kuwa na wagonjwa wengi
wa sikoseli na kama hatapata ufumbuzi wa kukabiliana nao mapemna asilimia
tisini na tano ya watoto watakaozaliwa wanaweza kufa kabla ya umri wa miaka
mitano.
“nadhani ni wakati muafaka kwa makampuni, wawakilishi wa nchi
mbalimbali na wadau wa sekta ya afya kuja kuunga mkono mapambano haya ya
sikoseli nchini,’ alisema
Dkt Makani aliongeza kuwa hospital ya Muhimbili wamefungua kitengo
maalum kwa ajili ya kuhudumia watoto wanaozaliwa na ugonjwa huo kwa msaada wa
mashirika mbalimbali ikiwemo la Welcome Trust kutoka Uingereza ambao
wanawapatia kiasi cha dola za kimarekani 250,000 kwa mwaka
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Little Fingers Music, Veronica Eyakuze
alisema kwamba shirika lake la mafunzo ya muziki limeamua kusaidia watoto wenye
matatizo na ugonjwa huo kwa njia ya kufundisha kupiga muziki, piano, gitaa na
kazi zingine za muziki katika kuhamasisha mapambano dhidi ya ugonjwa huo
“sisi katika Little Fingers Music tupo mstari wa mbele katika mapambano
dhidi ya ugonjwa huo kwa miaka mingi na kusaidia watoto wenye matatizo hayo kwa
kuwafundisha kupiga muziki ili wajue kwamba wanaweza kufanya shughuli yeyote na
kuibua vipaji vyao,’ alisisitiza
Mkurugenzi wa Kituo cha Little Fingers Music, Veronica Eyakuze akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo. |
Naye Arafa Said Salim (27) binti aliyezaliwa na ugonjwa huo, alisema
kwamba ameanzisha taasisi yake ya kupambana ugonjwa huo kwa ajili ya
kuhamasisha jamii kwamba ugonjwa huo unaweza kuishi nao bila matatizo yoyote.
“nimeanzisha taasisi yangu ya Wagonjwa waishio na Sikoseli Tanzania
katika juhudi zangu binafsi za kuelimisha jamii kwamba ni muhimu kujua mapema
na kuweza kuishi na ugonjwa katika maisha ya raha na marefu,” alisema Arafa alisema kwamba yeye binafsi ameolewa na anaweza kuishi na mumewe
bila matatizo yoyote na ana matumaini anaweza kupata mtoto asiye na ugonjwa
huo.
Aliongeza pia kwa miaka takribani kumi tangu kitengo cha sikoseli
kufunguliwa katika hospitali ya Muhmbili utafiti umeonyesha kwamba vifo vya
watoto chini ya miaka mitano vinapungua.
Mwisho.
Post a Comment