Askari sita wa Kikosi cha Usalama Barabarani katika wilaya za Rungwe na
Mbeya waliofahamika kwa majina Coplo Johnson, PC Raymond, PC Simona, PC
Shaaban, PC Kajolo na Sajini Hezron, wamefukuzwa kazi kwa tuhuma za
kushawishi, kuomba na kupokea rushwa, blogu ya Mbeya Yetu imeripoti.
Kamanda
wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi amenukuliwa akisema kuwa askari hao
walifikishwa katika Mahakama ya Kijeshi na Hukumu kutolewa Aprili 24
mwaka huu na adhabu yao ikawa ni kufukuzwa kazi.
Aidha, askari
wengine waliofukuzwa kazi hivi karibuni ni pamoja na PC James Kagomba
aliyehukumiwa kifungo cha miaka 30 kwa kosa la wizi wa kutumia silaha.
WP Prisca Kilwai anayekabiliwa na kesi ya wizi wa mtoto.
DC
Marcelino Venance Na. 8084, PC Juma Idd Na. 3117 na askari mgambo MG
Jackson Mwakalobo waliohukumiwa kifungo cha mwaka 1 kwa kosa la
kusababisha kifo cha Dentho Kajigili, aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya
Sekondari Ivumwe, Mbeya.
Chanzo cha habari na mtandao wa www.wavuti.com
Post a Comment