Wakuu wake walichukua
hatua ya kumuonya polisi huyo baada ya picha yake kusambazwa kwenye mitandao ya
kijamii na kupigiwa gumzo kubwa.
Alipigwa picha akiwa
amevalia sketi yake fupi na yenye kumbana akiwa anashika doria katika eneo
ambako mashindano ya magari yalikuwa yanafanyika eneo la Kati mwa Kenya.
Afisa huyo kwa jina
Linda Okello, alitakiwa kufika mbele ya Mkuu wake James Mugeria na kuonywa
vikali dhidi ya kuvalia hivyo kwa mara nyingine, kitendo ambacho alifahamishwa
kuwa ni utovu wa nidhamu kwa kuvalia nguo isiyo ya heshima kwa polisi
Maafisa mjini Kiambu
wamesema kuwa kupewa onyo kwa afisa Linda na kuonywa dhidi ya kuvalia sketi
yake iliyokuwa imembana sana ni jambo la kawaida na kwamba ameruhusiwa
kuendelea na majukumu yake.
Waliongeza kuwa afisa
huyo ameamrishwa kuanza kuvalia kiheshima.
Alipigwa picha na
mwanahabari mmoja wa gazeti moja maarufu nchini Kenya akiwa na wenzake kazini
mjini Kiambu. Lakini punde si punde picha hiyo ikaanza kusambazwa kwa mitandano
ya kijamii na baadhi wakiikejeli.
Taarifa ya polisi huyo
kuonywa ilizua hasira kwenye mitandao ya kijamii baadhi wakihoji ikiwa ni
makosa kwa afisaa wa polisi kuvalia sketi ya kumbana. Nini Kauli yako?
Post a Comment