Timu ya mpira ya Barcelona ya uhispania na mabingwa watetezi wa ligi hiyo  imepigwa stop na shirikisho la soka la kandanda duniani FIFA kushiriki katika  kufanya uhamisho wa mchezahi yeyote kwa kipindi cha misimu miwili ya usajili mpaka hapo June 2015.

Hii inatokana na  mara baada ya timu hiyo kugundulika ya kwamba imekuwa ikikiuka  taratibu za uhamisho kwa wachezaji chini ya miaka 18 wasiokuwa wazaliwa wa uhispania.
Lionel Messi mmoja katijka ya wacheaji waiosajiliwa wakiwa na umri mdogo, akiwa na miaka 13

Timu hiyo na shirikisho la soka la nchi hiyo vyote kwa pamoja wamekutwa kukiuka taratibu hizo kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2009 hadi 2013 na hivyo shirikisho hilo kusubiria adhabu yake pia.

Katika uchunguzi huo ulifanywa dhidi ya baadhi ya wachezaji wenye umri mdogo waliosajiliwa na timu hiyo na kushirikia baadhi ya michuano kwa kipindi toka 2009 hadi 2013.

Katika uchunguzi uliochukua takirbani mwaka mzima, maofisa wa FIFA wamegundua ya kwamba timu hiyo imekuwa ikikiuka taratibu zinapaswa kufuatwa katika uhamisho wa wachezaji wa kigeni.

Wachezaji wa kimataifa walio chini ya miaka 18  wanaovuka mipaka huwa wanapaswa kusajiliwa kwa kufuata taratibu maalumu na chini ya taratibu maalumu za ziada.

Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.