Timu ya Liverpool imezidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa Ligi kuu ya uingereza na kuzidi kufufua matumaini yake ya kuchukua ubingwa wa Ligi kuu ya Uingereza mara baada ya miaka 24 tangia ilipofanya hivyo kwa mara ya mwisho mnamo mwaka 1990.
Katika mchezo wa jana ambapo ulishuudia timu hiyo ikibwaga timu iliyokuwa inapewa nafasi kubwa ya kunyakua ubingwa huo timu ya Manchester City na hivyo kufikisha pointi 77 na kuiacha Manchester City kwa point saba ila ikiwa mbele kwa michezo miwili na mbili zaidi ya timu inayoshika nafasi ya pili, Chelsea ambayo ina pointi 75 wakiwa na mechi sawa.
Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard ilibidi kutokwa machozi mara baada ya timu hiyo kukaribia kabisa na hatua ya kuchukua ubingwa huo. Magoli ya awali yaliofungwa na Raheem Sterling na Martin Skrtel yaliiwezesha timu hiyo kuwa katika hali nzuri ya kushinda mpambano huo uliokuwa muhimu kwa timu.
Mchezaji toka Ivory Coast na tegemeo kwa timu ya Manchester United, Yaya Toure akitoka uwanjani kwa maumivu. |
Post a Comment