Ndege ya Kenya Airways safari namba KQ-482, iliyokuwa ikitua katika
uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam iliacha njia
(runway) kabla ngazi za dharura kufunguka na waliokuwa ndani kulazimika
kutoka kwa dharura.
Mmoja wa abiria wa KQ482 akisaidiwa kutoka katika ndege huyo huku ngazi za dharura “chute” zikiwa zimefunguka. Picha na Miguel Martinez. |
Waliokuwepo eneo la tukio wanasema injini moja ya ndege hiyo aina ya
Embraer E190,iliyokuwa safarini kutoka Nairobi kwenda Dar Es Salaam,
ilipata hitilafu (engine failure) na kukosa nguvu (thrust) ya kusimama
katika hali ya kawaida huku mvua kubwa ikinyesha. Ingawa uchunguzi
utatoa jibu kamili.
Akizungumza na Taarifa News, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa
Anga Tanzania (TCAA) Fadhili Manongi, amethibitisha kutokea kwa mkasa
huo na kueleza kuwa halikuwa tatizo kubwa na kwamba abiria na
wafanyakazi wa ndege hiyo wako salama.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Fadhili Manongi |
Hata hivyo walioshuhudia na baadhi ya abiria waliokuwemo katika
chombo hicho wamenukuliwa wakisema walipata mshtuko na wengine majeraha
madogo.
Ndege kadhaa za safari za ndani na pia kimataifa ziliagizwa kutua
Zanzibar wakati tukio likishughulikiwa, kabla ya ndege kuvutwa na
kuwekwa sehemu salama na uwanja kufunguliwa upya.
Embraer ni ndege inayotengenezwa Brazil, na wataalam wanasema aina hiyo ya dharura si jambo la ajabu.
Post a Comment