Wito huo umetolewa na Afisa kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Valerian Vitalis Kidole katika semina ya siku nne kwa waandishi wa habari na watangazaji wa redio jamii iliyomalizika mwishoni mwa katika ukumbi wa Kartasi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Kidole alisema kuwa
ili kuhakikisha jamii inapata lishe haina budi kutumia vyakula vile
vinavyopatikana katika maeneo wanamoishi kuliko kusubiri vyakula vya msaada
kutoka serikalini na vyakula kutoka viwandani.
Hayo yamezungumzwa
katika mafunzo ya Kupunguza Madhara ya Maafa na kutoa Msaada wa Dharura
yaliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa kushirikiana na
UNESCO kwa ajili ya waandishi wa Habari na watangazaji wa redio jamii
yanayofanyika Kahama wakati mwezeshaji akitoa mada ya Usalama wa Chakula
nchini.
Serikali kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali wa chakula hutoa msaada wa chakula kwa
wananchi pale kunapotokea upungufu wa chakula katika maeneo husika.
Aidha Kidole amesema
kuwa chakula cha msaada kinachotolewa na serikali ni nafaka ambayo
hayawezi kuboresha afya zao.
Katika halmashauri za
mikoa nchini ambazo zina upungufu wa chakula, viongozi wa ngazi husika
hawana budi kuwaelimisha wanachi juu ya kulima mazao mengi yanayohimili hali ya
hewa husika na kwa wakati mwafaka ili kupunguza tatizo la upungufu wa chakula
katika maeneo yao. Ni kwa namna hiyo jamii itaipunguzia serikali mzigo wa kutoa
chakula cha msaada na badala yake kufanya shuguli nyingine za maendeleo.
Afisa
kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Valerian Vitalis Kidole,
akiendesha mafunzo ya siku nne ya wanahabari na watangazaji wa redio jamii
yaliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa kushirikiana na
UNESCO yaliyofanyika katika ukumbi wa Kartasi uliopo wilayani Kahama Mkoani
Shinyanga.
|
Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Mama Rose
Haji Mwalimu, akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari na watangazaji wa Redio
jamii ya namna ya kuandaa jedwali maalum kwa ajili ya kuibua masuala katika
utayarishaji wa vipindi kwenye mafunzo ya siku 4 yaliyomalizika mwishoni mwa
juma mjini Kahama.
|
Msimamizi wa huduma za hali ya hewa kwa jamii kutoka
Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA), Hellen Msemo, akitoa mafunzo ya
namna ya kuripoti taarifa sahihi za hali ya hewa kwa jamii kwa jamii na kuwaasa
kuepuka upotoshaji wa taarifa za uongo kutoka kwenye vyombo visivyohusika zaidi
ya mamlaka hiyo
|
Baadhi ya waandishi na watangazaji wa redio za jamii
nchini wakifuatilia kwa umakini mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Shirika la
Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa kushirikiana na UNESCO ambayo yamemalizika
mwishoni mwa juma mjini Kahama.
|
Mwandishi wa Redio Jamii ya Pambazuko FM, Goodluck
Msowoya, akielezea uzoefu wake kwa washiriki wenzake wakati wa mafunzo hayo
ambapo amewataka kuwa na uthubutu kwa manufaa ya jamii.
|
Mwandishi wa Redio Jamii ya Pangani FM, Mwajabu Ali
akiwasilisha kazi ya vikundi wakati wa mafunzo hayo yaliyomalizika mwishoni mwa
juma mjini Kahama.
|
Washiriki wakiwa katika vikundi kazi |
Post a Comment