MVUA zinzazoendelea kunyesha katka maeneo mbalimbali ya nchi na takribani jijini Dar Es Salaam katika siku tatu zilizopita na za leo hii zimezidi kuharibu miundombinu ya sehemu
kubwa la jijini Dar es Salaam na vitongoji vyake achilia mbali sehemu nje
kidogo ya jiji hili mkoa wa pwani ambao daraja la Ruvu liliharibika na kuleta
adha kubwa watumiaji wa barabara hiyo ya morogoro road.
zikiwa zikichagizwa pia na miundo mbinu hafifu au mibovu hasa katika ya jiji la Dar Es Salaam kama ilivyoshuhuhudiwa leo hii na mwandishi wa habari hii katikati ya jiji katika eneo la Posta mpya karibu na stendi za mabasi yaendayo mwenge ambapo mvua iliyoshesha kwa takribani dakika kumi (saa sita na dakika 20 hadi sita na nusu) na kuacha maeneo hayo yakiwa taabu tupu kwa waendao kwa miguu na waendeshao vyombo vya moto.
Mvua iliyoyesha leo majira ya sita mchana kwa takribani dakika 15 na kufanya eneo hili la posta mpya kushindwa kupitika |
Kimsingi kero imekuwa kubwa kuingia katika ya jiji la Dar es Salaam na
kutoka kwa sababu ya foleni ya magari na mifereji yote ya maji imezibuka kwa
hiyo ni maji kila kona ya mtaa kati kati ya Posta na Kariakoo.
Ingawaje, wizara ya Ujenzi imesema kuwa asilimia kubwa ya miundombinu
iliyoharibiwa na mafuriko haikujengwa chini ya kiwango kama inavyodaiwa, bali
ni matokeo ya uharibifu wa mazingira.
Akizungumza na moja ya gazeti la kila siku hapa nchini, Msemaji wa
wizara hiyo, Martin Ntemo amesema madaraja mengi yaliyoharibiwa na mvua
zinazoendelea nchini yameliwa katika makutano na barabara na si kumeguka.
“Mito mingi imechepuka katika mikondo yake ya zamani kutokana na
uharibifu wa mazingira unaofanywa na wakazi wa maeneo hayo kila kukicha.,” amesema
na kuongeza:
“Pia asilimia kubwa ya madaraja hayo yameshuka katika urefu wake wa
awali kutokana na mchanga unaosababishwa na mmonyoko wa udongo, hivyo kupunguza
sehemu iliyokuwa imekadiriwa kwa maji kupita.”
Mvua ya dakika kumi tano iliyonyesha leo na huu nndiye hali halisi ilivyokuwa kwa watumia barabara hiyo wa miguu na wa magari |
Aliongeza kuwa madaraja na barabara hizo nyingi zilikuwa
zimeshakabidhiwa muda mrefu kwa Serikali na kwamba Wizara inaendelea kutafuta
suluhu ya kuyarudisha katika hali yake ya kawaida.
Mvua zinazoendelea kunyesha nchini zimeendelea kuharibu miundombinu
mbalimbali ya barabara ambapo mawasiliano kati ya Jiji la Dar es Salaam na
mikoani yalikatika kutokana na madaraja kuharibika na kufurika maji.
Mvua iliyonyesha leo jumatano majira ya sita mchana, uonekano wa eneo hili maaruf kwa magari ya mwenge posta |
“Tulikuwa na wakati mgumu katika Daraja la Mpiji kutokana na uhaba wa
mawe, lakini tayari tumeshapata sehemu ambayo malori yatakuwa yakichukua na
kupeleka eneo la ujenzi,” amesema Ntemo.
Amesema walifanikiwa kupata mawe eneo la Wazo Hill na viunga vyake
ambayo yatasaidia kukamilisha ujenzi wa daraja hilo lililopo Barabara ya
Bagamoyo kufikia leo asubuhi au mchana.
Mwisho
Post a Comment