Timu za Barcelona na Manchester United jana zilitupwa nje rasmi katika mashindano ya klabu bingwa ya ulaya mara baada ya kufungwa katika michezo yao ya marudiano katika michezo za robo fainali.
Katika michezo iliyopchezwa jana usiku ilishuhudiwa mabingwa hao watetetezi wa ligi kuu ya Uingereza wakifungwa jumla ya mabao 3-1 na kufanya tmabingwa watetezi wa michuono hiyo kushinda jumla ya mabao 4-2 kwani katika mchezo wa awali uliochezwa jijini Manchester timu hizo zilitoshana nguvu kwa jumla ya mabao 1-1. Na mabigwa wa Laliga timu ya Barcelona ilishuhudia ikiaga michuano hiyo maa baada uya kukubali kufungwa na timy ya Atletico Madrid katika mchzo mkali uliochezwa katika uwanha wa Vicente Calderon jijini Madrid na kuifanya timu hiyo kusonga mbele kwa jumla ya mambo 2-1 kwani katika mchezo wa awali uliofanyika Nou Camp timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
Kwa matokeo hayo zimeziacha timu za Real Madrid , Atletico Madrid zote kutoka jiji moja la Madrid la Uhispania, Bayern Munich ya Ujerumani na Chelsea ya Uingereza zikisonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali mara baada ya mechi zao za juzi na jana.
|
Timu za Atletico Madrid na Barcelona zikiwa zimejipanga kabla ya kuanza kwa mchezo wa jana katika uwanja wa Vicent Calderon. |
|
Kocha mkuu wa Atletico Madrid, Diego Simeone |
|
Wacehzaji wa Manchester United wakiwa wanatoka uwanjani vichwa chini mara baada ya kuaga michuano hiyo |
|
Kocha mkuu wa Machester United, DAvid Moyes aliyesema makosa ya kizembe ndio yaliyosababisha kutolewa kwenye michuano hiyo |
Post a Comment