Oparesheni Nzito ya kuzuia Bodaboda na Bajaji zisifanye safari zake kutoka Mwenge na maeneo mengine kuelekea mjini Posta imechukua sura mpya leo baada ya Askari wa Usalama wa Barabarani kuanza kukamata Bodaboda na Bajaji zote zinazovuka Mwenge kuelekea Posta, Zoezi hilo ambalo limefanyika Mwenge Mataa Jijini Dar limeendelea kufanyika na kufamikiwa kuwanasa wengi.
Oparesheni Kamata Bodaboda na Bajaji ikiwa inaendelea upande wa Mwenge mataa ambapo Bajaji nyingi zimekamatwa. |
Kwa mujibu wa Msemaji na Muongozaji wa
Oparesheni hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema kwamba wameamua
kufanya hivyo ili kuzuia Msongamano wa Magari pamoja na bodaboda pia Bajaji
kuelekea Mjini Posta, Aliongeza kuwa kumekuwa na uhalifu sana wa Silaha
unaotumiwa na bodaboda hasa maeneo ya mjini hivyo ndio maana wameamua kuzuia.
Askari wa Usalama wa Barabarani akiwa anawaandikisha Baadhi ya Bodaboda na Bajaji wenye makosa mbalimbali ili waweze kulipia tozo pamoja na kupelekwa kituo cha Polisi |
“Tumefanya hivi ili kuepusha msongamano
kuelekea Posta, lakini pia kumekuwa na uhalifu sana unaotumiwa kwa njia ya
Bodaboda hivyo tunafanya oparesheni hii ili kupunguza tatizo hili. Tulicho
kifanya tumewaruhusu kufanya safari pembezoni mwa mji tuu hivyo Eneo la Mwenge
kwa sasa Limeingia katika zone ya eneo la Mjini,Kama tuliweza kuzuia Daladala
ndogo”Hiace” pia na hawa watakuja kuelewa ingawa ni zoezi gumu na linalo hitaji
elimu ya ziada ambayo tumesha anza kuwapa na tunaendelea kuwapa”
alimalizia kwa kusema “Pia hii ni Oparesheni ya kawaida tuu ya kukamata wale
ambao hawana Leseni za kuendesha vyombo hivi pamoja na makosa mbalimbali”
alisema Polisi huyo.
Baadhi ya Bodaboda na Bajaji wakiwa wanangojea Hatma yao baada ya kukamatwa. |
Kwa mujibu wa madereva wa Bodaboda na Bajaji
wamesema kwamba huo ni uonevu kuwakataza wao wasiweze kwenda Mjini kwani na wao
wanatafuta ridhiki yao na wameomba Serikali iwasaidie wapatiwe njia mbadala ya
wao kwenda maeneo hayo.
Wanao ruhusiwa kwenda Posta na Bajaji au
Bodaboda ni wale ambao ni wamiliki binafsi na wanatakiwa wapite njia hizo
wakiwa Bila abiria yoyote.
Madereva wa Boda Boda na Bajaji wakipata maelezo ya kina ya kwanini wamezuiliwa kwenda Posta wakitokea Mwenge. |
Dereva huyu akiwa amejawa na masikitiko kibao mara baada ya bodaboda yake kukamatwa katika operasheni hiyo. |
Habari na Picha kwa msaada wa blogu ya Moblog.
Post a Comment