RAIS Jakaya Kikwete amewahakikisha watanzani serikali ipo katika hatua za mwisho kuandaaa sheria, kanuni na utaratibu kwenye sekta ya gesi na mafuta kwa ajili ya uwekezaji wenye tija nchini.
Akizungumza kwenye kongamano la 19 la mwaka
kwenye uzinduzi wa ripoti ya ya utafiti wa Shirika Lisilo kuwa la Kiserikali la
(REPOA) linalofanyika jijini Dar es
Salaam kwa siku mbili, Rais kikwete alisema mpaka mwezi oktoba mwaka huu
serikali itakuwa imeweka sheria, kanuni kwenye sekta ya gesi na mafuta ili
wazawa washiriki kikamilifu.
Rais wa Tanzania Mheshimiwa, Dakta Jakaya Kikwete |
“mpaka ukifika mwezi Oktoba basi sheria na
taratibu zote zitakuwa tayari na kufungua milango pia kwa wawekezaji wa ndani
kushiriki kwenye sekta ya gesi na mafuta nchini,” alisema
Alisema kwamba kwenye uwekezaji wa gesi na
mafuta taifa litapata manufaa makubwa na mabilioni ya pesa yataingia kwa hiyo
ni nafasi muhimu pia kwa watanzania wenye biashara za kati na ndogo ndogo kunufaika
na uwekezaji huo.
Rais Kikwete alisisitiza kwamba katika uwekaji
wa sheria na taratibu lazima mambo ya urasimu na rushwa viondolewe mara moja
ili kuhakikisha sekta hiyo inakuwa na manufaa kwa wananchi wote.
Aliongeza kwamba lazima serikali na wadau wote
muhimu wajiridhishe kwamba hakuna wizi wala utapeli katika sekta gesi na mafuta
ili kumletea mwananchi wa kawaida maendeleo.
Kikwete alifafanua kwamba lazima serikali
ihakikishe inajipanga vizuri ili kuzuia vitendo vyovyote vya hujuma, wizi na
rushwa ili kuleta matokeo chanya kwa nchi na watu wake.
Alisema kwamba kwa muda mrefu watafiti wa ndani
wamekuwa na msaada mkubwa katika kuisaidia serikali kutambua maeneo yenye
mahitaji zaidi na hasa katika kuboresha maisha ya wananchi na kupambana na
tatizo la ajira nchini.
“tafiti hizi za kila mwaka zimekuwa na msaada
mkubwa kwa wafanyabiashara wadogo wadogo, wakulima na wananchi wa kawaida
katika kufanya uamuzi sahihi kwenye maeneo,” aliongeza, Alisema kwamba nchini Tanzania zipo ajira ndogo
ndogo milioni tatu lakini wanaofanya ajira hizo ni milioni tano na laki mbili
kati hao asilimia 64 ni wanawake.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA,
Profesa Samwel Wangwe alisema kwamba tafiti hizi zinalenga kuwasaidia wananchi
wanaojishughulisha na biashara ndogo ndogo ili kupunguza umaskini.
Profesa Wangwe alisema kwamba malengo ya tafiti
pia ni kuongeza tija kwa kupata uzoefu kutoka nchi mbalimabali ulimwenguni ya
jinsi ya kujenga viwanda, kusindikaji wa chakula na kupambana na tatizo la
ajira hasa kwa vijana na wanawake.
Aliongeza pia kwamba REPOA wamewaalika wataalamu
mbalimbali kutoka nchini ya Japan ili watanzania waweze kujifunza kutokana na
nchi zao katika harakati za kupambana umaskini Afrika.
Mwisho.
Habari na Mtandao wa Habari wa Makangale Satellite
Tanzania
Post a Comment