RAIS Jakaya Kikwete ametoa maagizo ya haraka ya utayarishaji mpya wa mfumo (Procurement) wa ulinzi katika viwanja vyote vya ndege nchini katika harakati za kudhibiti usafirishaji na uigizaji wa madawa ya kulevya Tanzania. Makangale Satellite inaripoti.
Rais Kikwete alitoa rai hiyo katika hafla ya uwekaji wa jiwe
la msingi katika mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria Julius Nyerere
International Airport (JNIA) jijini Dar es Salaam kwa kusema inakera sana kuona
wasafirishaji wa dawa za kulevya kukamatwa Afrika ya Kusini.
Rais
Kikwete akisisitiza jambo baada ya kuona uchoro wa jengo jipya la abiria na
mfumo wa ulinzi kutoka, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Injia
Suleiman Suleiman mwenye tai nyekundu
|
“sisi wengine tunaumia sana kusikia msanii fulani au
mwanamuziki kukamatwa na dawa za kulevya nchini Afrika Kusini, mtu unajiuliza
kapitaje hapa uwanja wa ndege dar au kwa kuwa msanii tu lakini inakera na
ninaumia sana,’ amesema Rais Kikwete amesema lazima mamlaka za viwanja vya ndege kwa kushirikiana
na wizara na wadau wengine waunganishe nguvu zao katika kupambana tatizo hili
la dawa za kulevya kwa kuwa linaichafua nchi nzima kimataifa na kikanda.
Rais
Kikwete na Waziri Mwakyembe wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi
mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo
jipya la abiria (Terminl Three)
|
Rais Kikwete aliongeza kwamba lazima mamlaka zinazohusika
zianze mara moja kutengeneza mfumo madhubuti wa ulinzi katika viwanja vya ndege
hasa wa Dar es Salaam na KIA kule kilimanjaro ambazo ndio njia kuu za
usafirishaji wa madawa hayo.
Amesema lazima kasi ya kupambana na usafirishaji na uigizaji
wa dawa za kulevya kupitia viwanja vya ndege iongeze na siyo kusuasua miaka
miwili au mitatu ya kutengeneza mifumo ya ulinzi ya kimataifa.
Rais Kikwete amesema kwamba kama kuna watumishi wa idara ya
forodha (TRA), Mambo ya Ndani au Polisi wanaoshirikiana na wauza madawa ya
kulevya apewe majina yao na watashughulikiwa mara moja.
“tusimuonee haya mtu yeyote hata kama ni mtumishi wa umma
kwa sababu tunaonekana wote tunajishughulisha na biashara hiyo haramu ni lazima
tuchukue hatua madhubuti,” aliongeza Rais Kwa upande wake, Waziri wa Uchukuzi, Dkt Harrison Mwakyembe
akizungumza na mwandishi wa habari hizi muda mfupi baada ya Rais kuweka jiwe la
msingi amesema kuwa tayari Mamlaka ya viwanja vya ndege (TAA) wameshaweka
mifumo hiyo yaani (Procurement) katika kudhibiti dawa za kulevya.
Amesema kuwa katika jengo jipya la abiria (Terminal three)
kuna hatua tano za kukagua madawa ya kulevya na aina nyingine ya vitu
visivyoruhusiwa katika uwanja wa ndege kwa hiyo serikali imejipanga kumaliza
kabisa tatizo hili nchini.
“kimsingi mifumo hii ipo tayari katika jengo hili jipya la
abiria na kama kuna mtu atapitisha dawa za kulevya basi nitampa zawadi ya
fedha,’ amesema Dkt Mwakyembe
Dkt Mwakyembe alisisitiza kwamba katika mapambano dhidi ya
dawa za kulevya lazima wizara na TAA watashirikiana na wadau wengine kama vile
Mamlaka ya Mapato (TRA) kupitia idara ya forodha, wizara ya mambo ya ndani
yaani Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa (TISS).
Hayo yanakuja wakati taarifa zilizopo ni kwamba
wasafirishaji wa dawa za kulevya kuanza kutumia fukwe ndogondogo za bahari
nchini kuziingiza kutoka Mashariki ya mbali.
Mwisho.
Post a Comment