|
Mshehereshaji ambaye ni
Mwanakamati ya maandilizi ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya
Habari Duniani 2014, Usia Nkhoma Ledama akiwatambulisha baadhi ya
waandishi wa habari wakongwe (hawapo pichani) kwa mgeni rasmi Jaji
Mstaafu Mark Bomani.(Picha zote na Zainul Mzige). |
Jaji Mstaafu Mark Bomani amesema lengo
la mchakato wa Katiba ni kuhakikisha kwamba Tanzania inapata Katiba ambayo ni
bora zaidi kuliko zote itakayoshughulikia changamoto na kuweka mazingira ambayo
yatamrahisishia maendeleo mwananchi kwa haraka.
Akitoa risala katika maadhimisho ya Siku
ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani leo katika ukumbi wa Kimataifa wa
Mikutano wa AICC jijini Arusha, Jaji Mstaafu Mark Bomani, amesema jukumu la
mwanahabari ni kuwaelimisha baadhi ya wabunge wa Bunge Maalum la Katiba ambao
hawana uelewa mkubwa na mchakato wa Katiba hawajui maana halisi ya Katiba mambo
ambayo yanasababisha kujadili Katiba hiyo kwa maneno mabaya, kutishiana, matusi
na kejeli.
|
Baadhi ya waandishi wa habari wakongwe (Ma-veterans) wakimsalimia mgeni rasmi. |
“Zoezi la mchakato wa Katiba ni kubwa na
wabunge wengi wa Bunge Maalum la Katiba hawaelewi wajibu wao katika
kuijadili Katiba hiyo matokeo yake ndio hayo wanayoshuhudia Watanzania”.
Mara nyingi Watanzania wameshuhudia
mijadala ya kejeli, malumbano, matusi, kudharauliana pale hoja zinapojengwa na
upande ambao haukubaliki na upande mwingine jambo ambalo limewavunja moyo
Watanzania na kutokuwa na imani ya kupata Katiba inayolenga kumlinda mwananchi.
Jukumu la wanahabari ni kutoa elimu ya
kutosha kuhusu yaliyomo katika Katiba Mpya na kuandika habari za maendeleo ili
majadiliano yatokanayo yawe endelevu yamtendee haki mwananchi wa kawaida kwa
lengo la kuboresha maisha yao.
|
Meza Kuu, kutoka kushoto
ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Elimu, Sayansi na Mawasiliano ya Umoja
wa Mataifa (UNESCO) Bw. Abdul Wahab Coulibaly, Mkurugenzi wa Mfuko wa
Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) Bw. Ernest Sungura, Mkuu wa Wilaya ya
Arusha, Bw. John Mongela, Mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mark
Bomani, Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika,
Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Bw. Mohamed Tibanyendera, Rais wa Umoja wa
Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Kenneth Simbaya
na Meneja Utafiti na Ushapishaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw.
John Mirenyi. |
“Inasikitisha kuona kuwa hali ya
Mtanzania inazidi kudidimia au kubaki pale pale katika sehemu nyingi hasa
vijijini katika kipindi cha miaka 40 iliyopita kwa kukosa fursa muhimu za
maendeleo na viongozi hawalioni hilo”, amesema Jaji Mstaafu Mark Bomani.
Wakati huo huo mgeni huyo rasmi amekemea
tabia ya kuandika habari za kuwasifu viongozi na kupokea Rushwa hali
iliyojitokeza katika miaka ya hivi karibuni na kusema kwamba ni fedhea kwa
tasnia ya habari kutofuata maadili ya uandishi.
Amesema kwamba nchi itaendeshwa kwa
kusimamia haki na ukweli na kuwataka wanahabari wasichoke kuisimamia haki na
uhuru wa nchi yao bila woga kwani bila kufanya hivyo nchi itaongozwa kiimla.
|
Mgeni rasmi Jaji Mstaafu
Mark Bomani, akitoa risala wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa
Vyombo vya Habari Duniani 2014 yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano
wa kimataifa wa AICC jijini Arusha mwishoni mwa juma |
“Kuna tabia ya vyombo vya habari ya
vyombo vya habari kununuliwa ili visiandike au kufichua maovu ni fedhea kwani
vyombo vya habari ni kioo cha jamii”.
Akizungumzia kuhusu sheria za habari za
mwaka 2007 na 2008, Jaji Mstaafu amesema ni aibu kuona mswaada wa sheria ya
habari umekwama kwa zaidi ya miaka 10 kwa sababu ambazo hadi leo hazijaeleweka.
Amewataka waandishi wa habari wasikate
tamaa na badala yake waendelea na kupambana kuhakikisha kwamba harakati za
kupata Sheria ya Haki ya Kujua inafanikiwa ili kupunguza matukio ya manyanyaso,
kupigwa, kuteswa, kufungwa kwa vyombo vya habari na kuuwawa.
“Haki haiyombwi simamieni Haki zenu na
songeni mbele”, ameongeza Jaji Bomani.
|
Sehemu ya wadau wa tasnia ya Habari wakisikiliza risala ya mgeni rasmi. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Arusha,
Bw. John Mongela akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa wa Arusha
kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani
yaliyofanyika jijini Arusha kenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa
AICC |
|
Mwenyekiti wa Taasisi ya
Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Bw.
Mohamed Tibanyendera, akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa
Vyombo vya Habari Duniani 2014 yaliyofanyika kwenye ukumbi wamikutano
wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha. |
|
Wageni waalikwa na wadau wa tasnia ya habari wakiwa kwenye ukimya kumkumbuka Mwandishi aliyeuwawa mkoani Iringa Daudi Mwangosi. |
|
Mkurugenzi wa Shirika la
Elimu, Sayansi na Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa (UNESCO) Bw. Abdul
Wahab Coulibaly, akitoa Ujumbe wa Pamoja wa Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Irina Bokovas kuhusiana na Siku ya
Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014. |
|
Meneja Machapisho, Utafiti
na Uhifadhi Hati wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. John Mirenyi,
akitoa maelezo ya machapisho mbalimbali yaliyoandaliwa na baraza hilo
yakiwemo yenye madhila mbalimbali yaliwahi kuwakumba baadhi ya waandishi
wa habari ndani na nje ya nchi. |
|
Mkurugenzi wa Mfuko wa
Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) Bw. Ernest Sungura, akizungumzia
mchango wa mfuko huo unaowawezesha waandishi wa habari kutafuta habari
za uchunguzi na zinazoigusa jamii. |
|
Wasanii wa Bendi ya Mrisho
Mpoto (Mjomba Band) wakitoa burudani kwa wageni waalikwa wakati wa
maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014
yaliyofanyika jijini Arusha mwishoni mwa juma. |
|
Sehemu ya wadau wa tasnia ya habari wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini hapo. |
|
Katibu wa Chama cha
Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT), Henry Muhanika, akisoma
hotuba kwa niaba ya Dr. Reginald Mengi kwenye maadhisho hayo. |
|
Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Kenneth Simbaya, akizungumzia wakati wa maadhimisho hayo. |
|
Mwenyekiti wa Jukwaa la
Wahariri (TEF), Absalom Kibanda, akizungumzia changamoto mbalimbali
zinazowakumba waandishi wa habari wakati maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa
Vyombo vya Habari Duniani 2014 yaliyofanyika jijini Arusha |
|
Mkurugenzi wa TAMWA, Bi.
Valerie Msoka, akizungumzia changamoto za usawa wa Kijinsia katika
uongozi kwenye Vyombo vya Habari nchini. |
|
Meneja Uhusiano wa TANAPA,
Pascal Shelutete, akizungumzia ushiriki wao kwenye Siku ya Uhuru wa
Vyombo vya Habari Duniani 2014 ambapo aliwataka waandishi wahabari
kutumia kalamu zao vizuri katika kukuza Utalii wa Tanzania ndani na nje
ya nchi. |
|
Meneja Uhusiano wa Hifadhi
ya Taifa ya Ngorongoro, Bw. Adam Akyoo, akifafanua jambo wakati wa
maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014 ambapo
amewataka waandishi wa habari kutumia nafasi yao katika kupambana na
suala la Ujangili linaloendelea nchini. |
|
Mrisho Mpoto akiwafungua
vitambaa wasaani wa Mjomba Bendi kama ishara ya kuwapa Uhuru waandishi
wa Habari kuzungumza kilio chao mbele ya mgeni rasmi kama ujumbe wa Siku
ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014. |
|
Mrisho Mpoto na Bendi yake
akighani mashairi na kuelezea madhila wayapatayo waandishi wa habari
wawapo kazini ikiwemo usalama wao katika kazi zao za kila siku. |
|
Makamu wa Rais wa Umoja wa
Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC), Jane Mihanji
akimkaribisha mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mark Bomani kuzindua Video mpya
ya wimbo "Uhuru Wangu" wa Mrisho Mpoto uliokuwa kwenye Albamu yake mpya
inayoitwa WAITE. |
|
Mgeni rasmi Jaji Mstaafu
Mark Bomani, akibonyeza kitufe kuzindua rasmi wimbo huo wakati
maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014. |
|
Wageni waalikwa wakitiza wimbo huo. |
|
Mgeni rasmi kwenye
maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani Jaji Mstaafu
Mark Bomani akizindua na kuonyesha moja ya Ripoti ya Unyanyasaji dhidi
ya Uhuru wa Habari iliyoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT).
Kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika -
Taiw la Tanzania (Misa - Tan), Bw. Mohamed Tibanyendera |
|
MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo,
mkoani Pwani, Ahmed Kipozi akiteta jambo na mmoja wa Waandishi wa
Habari wakongwe Bw. Salim Salim kutoka visiwani Zanzibar. |
|
Waandishi wa Habari
wakongwe (Ma-Veterans) kutoka kushoto Mama Eda Sanga, Fatuma Aloo na
Leila Sheikh wakifurahi jambo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa
Vyombo vya Habari yaliyofanyika jijini Arusha . |
|
Mshauri na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Mama Rose Haji Mwalimu, akisalimiana na Meneja
Uhusiano wa Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, Bw. Adam Akyoo wakati
maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014
yaliyofanyika jijini Arusha. |
|
Wadau wa tasnia ya habari wakinunua Album ya msaanii Mrisho Mpoto. |
|
Baadhi ya wasanii wa Mjomba Band wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mwandishi wa habari mkongwe Leila Sheikh |
Post a Comment