KAMPUNI
ya simu za mkononi ya Tigo Tanzania, leo imezindua tamthilia ya ‘Kinga ya Moyo
Wangu’ itayokuwa inarushwa hewani kila siku kwa wiki nane na kituo cha utangazaji
cha Clouds FM ambacho kitatoa elimu na kuhamasisha watumiaji wa simu za mkononi
wa mtandao wa tigo kujiunga na bidhaa ya pona na Tigo bima.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo asubuhi jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa
Tigo, Diego Gutierrez amesema tamthilia hiyo maridhawa yenye matukio ya
kusisimua itawavutia wasikilizaji pamoja na kuwaelimisha watanzania kuhusu
manufaa ya bima.
“Kampuni
ya simu za mkononi kama Tigo ina wajibu katika kuwapatia wateja wake huduma na
bidhaa zenye gharama nafuu. Sambamba na jinsi teknolojia ilivyoweza kuleta
mageuzi katika namna ambavyo tunaweza kutuma na kupokea fedha barani Afrika,”
“hivi
sasa tupo tayari kufanya hivyo kupitia bima ya simu. Tigo inayofuragha kuwa
mstari wa mbele katika hatua hii kubwa kwa ajili ya Tanzania, ukuaji wa uchumi
wake na maendeleo ya taifa nzima,” amesema Gutierrez
Amesema
kwamba programu hiyo ya redio imefadhiliwa na benki ya maendeleo ya Umoja wa
Ulaya kwa ajili ya kuelimisha umma umuhimu na faida ya kuwa na bima wakati
wote.
Kwa
upande wake , Meneja Mkazi wa Bima Tanzania, Christian Karlander amesema kuwa
tamthilia hiyo itarushwa mara mbili kwa siku kwa muda wa wiki nane kupitia
vipindi vya Jahazi na Leo Tena.
“Mradi
huu umezinduliwa na Bima, Kampuni inayoongoza kwa kutoa bima kupitia teknolojia
ya simu za mkononi nchini Tanzania, ambayo inatoa huduma ya bima ya maisha nay
a kulazwa hospitalini jijini Dar es Salaam kupitia mtandao wa simu wa Tigo,”
amesema
Karlander
aliongeza kuwa takribani milioni 4.6 ambayo ni asilimia 19 ya watu wazima
nchini wamewekewa bima, lakini ni kupitia bima za waajiri wao au chini ya
mikopo hata hivyo, kiwango cha watanzania waliojiandikisha bima kwa hiari ni
ndogo sana.
“Jijini Dar es Salaam, Bima
imesajili zaidi ya wateja 500,000 baada ya miaka miwili tu ya kuanza kufanya
kazi nchini, na asilimia 79 ya wateja hao ni watu wenye vipato chini ya dola
2.50 (shilingi 4,215) kwa siku,” aliongeza Karlander
Alisisitiza kuwa bidhaa hiyo ya
bima kuanzia gharama ya shilingi 750 na kiwango cha juu ni shilingi za
kitanzania 4,000 kwa mwezi na Bima inalipa mpaka shilingi 600,000 pindi mteja
anapolazwa hospitalini au kufariki dunia.
Post a Comment