Julius amesema amefikia uamuzi huo wa kuomba kupatiwa mtu wa kumhudumia
kutokana na kutokuwa na mikono.
Amedai ulemavu huo, umesababisha pamoja na mambo mengine atumie mguu
wake wa kulia kuandika na kutandika kitanda.
Julius amefafanua zaidi kwa kusema ulemavu wake huo vile vile,
unasababisha ashindwe kuoga,kufua nguo zake na kwamba anapata taabu kubwa
wakati wa kujisaidia chooni.
"Kutoa madaftari na kalamu ndani ya mfuko,natumia mdomo wangu.Pia
kwa vile sina mikono natumia mdomo kuchukua chakula kutoka kwenye
sahani",amesema.
Julius anasema binafsi anamshukuru na kumpongeza rais Kikwete,kwa moyo
wake wa kuwajali walemavu wa aina mbalimbali.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ikungi wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida,Olivary Kamilly,akimsaidia mwanafunzi Julius Charels Kumvalisha soksi baada ya kutoka darasani |
"Nina imani kwamba kama ningeonana na Rais Kikwete kwa jinsi
anavyowajali walemavu mimi mwenye uchu mkubwa wa kujisomea ataweza kunisaidia
kupata mtu wa kunihudumia.Hata hivyo,sikati tamaa kusaidiwa na Rais wetu
Kikwete.Akisoma habari hii kwenye gazeti,nina hakika atanisaidia ili ndoto
yangu ya kufika chuo kikuu siku moja iweze kuwa kweli",amesema Julius.
Mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Ikungi mchanganyiko
wailaya ya Ikungi,Julius Charles,akitandika kitanda chake kwa kutumia mguu wake
wa kulia ambao pia anautumia katika kuandika.
|
Kwa mujibu wa mwalimu wake,Ana Mjema, Julius kwenye mitihani mbalimbali
huwa anashika nafasi ya tatu au ya nne.
Amesema mwanafunzi huyo asiye na mikono,kwa kutumia mguu wake ana
mwandiko mzuri kuliko wanafunzi wasio na ulemavu.Pia ana kasi katika kuandika.
Post a Comment