BENKI ya CRDB   imetenga kiasi cha zaidi ya shilingi  bilioni  moja katika bajeti  yake mwaka huu,  kwa ajili ya kuchangia katika  shughuli  mbalimbali za uboreshaji wa  huduma za kijamii  nchini.
Mkurugugenzi mkuu mtendaji wa CRDB, Dakta Charles Kimei
 Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Dokta Charles Kimei, alisema hayo kwenye hafla ya kukabidhi visima kwa shule  tatu za Msingi na Sekondari mkoani Singida  vilivyofadhiliwa  kwa benki hiyo.

Dk. Kimei alisema fedha zilizotumika kwa shughuli hiyo ni sehemu ya  zaidi ya shilingi bilioni moja  ikiwa  ni asilimia  moja ya faida  inayotengwa  na benki hiyo kila mwaka kusaidia huduma za jamii.

 
Alisema mwaka  jana, benki ya  CRDB ilipata faida ya zaidi ya shilingi bilioni 100 hivyo kulazimika kutenga kiasi hicho cha fedha  kama ilivyo sera yake ya kurejesha sehemu ya faida kwa wateja.
Kutokana na hali hiyo, Dk.  Kimei ametoa wito kwa wadau wengine kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha huduma za kijamii husani maji  safi na salama ambayo bado ni changamoto kubwa Vijijini.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Yahaya Nawanda, ameishukuru benki hiyo kwa kufadhili  uchimbaji na ujennzi wa visima hivyo, husani  kwa shule ya msingi Kizege yenye walemavu wa ngozi ambao walikuwa wakitembea umbali wa  zaidi ya kilomita 10 kufuata huduma hiyo.
Hata  hivyo   watoto hao albino licha ya kushukuru kwa msaada huo, wameomba kuunganishiwa maji  hadi kwenye mabweni yao badala ya kulazimika kufuata nje  suala ambalo ni hatari kwa maisha yao.
Pamoja na kufadhiliwa na CRDB na wadau wengine, shughuli  za uchimbaji na ujenzi  wa visima katika shule tatu za msingi na Sekondari mkoani Singida zimefanywa na Shirika la Nkwamira.

Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.