Singida. MKUU wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi, ameihimiza mamlaka ya usimamizi wa sekta ya hifadhi ya jamii (SSRA),kujituma zaidi katika kuhakikisha mifuko mbalimbali ya hifadhi ya jamii,inatoa taarifa sahihi kwa wananchi/wanachama watarajiwa juu ya haki zao,kabla hawajajiunga.
Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mwalimu Queen Mlozi |
Amedai kwamba wananchi/wanachama
watarajiwa,wakizitambua vema haki zao hizo,watakuwa wamejengewa uwezo wa
kufikia maamuzi sahihi katika kujiunga na mifuko hiyo ambayo Tanzania,ipo sita.
Mlozi ametoa rai hiyo jana
(12/5/2014) wakati akifungua semina ya siku moja iliyohusu uhabarisho wa
shughuli za mamlaka ya usimamizi wa sekta ya hifadhi ya jamii (SSRA),kwa wadau
mbalimbali wa mkoa wa Singida.
Alisema kwa vile SSRA inasimamia
mifuko yote hiyo sita ya hifadhi ya jamii ambayo ina mifuko tofauti tofauti,ina
jukumu kubwa la kusimamia mifuko hiyo inatoa taarifa za haki wanazopaswa kupewa
wananchi/wanachama watarajiwa,kabla ya kujiunga.
"Tumeshuhudia baadhi ya mifuko
ikipewa fursa ya kuwaeleza wananchama watarajiwa shughuli zao na mafao
wanayoyatoa,pindi watumishi hao wapya wakijiunga nayo",alisema Mlozi na
kuongeza;
"Hiyo ni hatua nzuri lakini
usimamizi na ufuatiliaji zaidi unahitajika kutoka mamlaka ya usimamizi, kwani
mifuko hii ya hifadhi ya jamii inatofautiana kwa maana ya uzoefu,mtandao wa
ofisi za matawi na watumishi na hata kwenye suala la uwekezaji".
Akiijengea nguvu hoja yake hiyo,
alisema suala la kutoa taarifa juu ya haki ya mwanachama mtarajiwa, ni kwa
mujibu wa sheria na 8 (nane) ya mwaka 2008 na kama ilivyorekebishwa mwaka 2012.
Alisema lengo kuu la sheria hiyo,
ni kwamba waajiri wachache wenye tabia ya kuwarubuni na kupindisha sheria na
kanuni, wasipate mwanya wa kutimiza azma au malengo yao.
Kwa upande mjumbe wa manejimenti na
mkuu wa ununuzi SSRA, Emmanuel Urembo, alisema kuwa hifadhi ya jamii ni haki ya
kila mtu na haki hii, imeainishwa katika ibara ya 11(1) ya katiba ya jamhuri ya
muungano wa Tanzania na sera ya taifa ya hifadhi ya jamii ya mwaka 2003.
"Haki hii pia imeainishwa
kwenye mkataba wa kimataifa wa haki za binadamu wa mwaka 1948 pamoja na
mikataba ya shirika la kazi duniani (ILO). Hii ni pamoja na masuala yote
ya msingi ya kijamii bila kujali hali ya kipato na michango yao au
ajira",alisema Urembo.
Post a Comment