Mgeni rasmi kwenye semina hiyo ya siku moja alikuwa ni Mlezi wa ATME,
kingunge Ngombale Mwiru ambaye alichukua nafasi hiyo kusema utafiti ndiyo utakaowezesha
kupiga hatua nzuri ya kupata tiba ya maradhi mbalimbali kwa kutumia tiba
asilia.
Mzee Kingunge alitumia muktadha huo kusema kuwa kuna dawa nyingi za
tiba asilia ambazo zina matokeo mazuri nay a haraka pengine kuliko zile za
kisasa, lakini hakuna utafiti wa kutosha nah ii ni kutokana na uhaba wa fedha
za kufanyia utafiti.
“tatizo kubwa linalowakabili watafiti wazalendo na hata hawa vijana wa
sasa kwenye vyuo vikuu vya tiba na uhaba wa fedha za kufanyia utafiti lakini
tukijikita kwenye utafiti maradhi mengi tunaweza kuyaondoa,” amesema Kingunge
Ngombale Mwiru
“Kushindikana kwa utafiti kwa sababu ya ukosefu wa fedha kunafanya
kukosekana maendeleo na badala yake tutakuwa tunarudia waliyogundua wazee wetu.
Tukitaka kwenda mbele lazima kusimamia waliyoyagundua wao na kuendelea mbele,”aliongeza.
Mkurugenzi kutoka Paseko T.H.P, Othman Shem.akielezea kuhusiana na Tiba Asili Tanzania na changamoto zake. |
Kingunge alisisitiza kwamba ili utafiti ufanyike, ni lazima wawepo watu
ambao wana taaluma hiyo na pia wapende fani hiyo na hali hicho ndicho
kilichozifanya India, China na Vietnam kupiga hatua katika tiba za asilia na
kupunguza kasi ya magonjwa mengi kwenye nchi zao.
“Mathalan, pumu katika hospitali inasemwa kuwa hakuna tiba yake zaidi
ya ile ya kutuliza, lakini mtaani unasikia kuna mtu anatibu pumu na pia kuna
watu wengi katika maeneo tofauti ambao wanatibu magonjwa mbalimbali, lakini
mwendelezo hakuna kwa kuwa hakuna mafungu ya utafiti.”
Amesema vijana wengi wasomi nchini wanafanya utafiti, lakini ni kwa
maelekezo ya taasisi za nje kwa kuwa zina fedha za kuwataka wafanye utafiti wa
hiki au kile kwa maslahi ya taasisi hizo za nje.
Kwa upande wake, Mwanasheria Onesmo Munuo akiwasilisha mada juu ya
mapungufu ya usimamizi wa sheria na 23 ya 2002 pamoja na kanuni zake na madhara
yanayotokana na udhaifu wa usimamizi huo amesema shirika la afya duniani
linakadiria kuwa Tiba Asili inatoa huduma kwa asilimia 80 ya wanaohitaji huduma
za afya katika nchi zinazoendelea.
“Hapa kwetu Tanzania inakisiwa kuwa asilimia 60 ya watanzania wanatumia
tiba asili katika kutibu magonjwa yao na kwamba kila kijiji kina watoa huduma
wa tiba asili,”
“hili linaonekana pia katika Sera ya Afya na Ustawi wa Jamii inaposema
kuwa takribani asilimia 60 ya wananchi huanza kutumia tiba asilia wanapopatwa
na maradhi kabla ya kwenda kwenye vituo vya kutolea huduma za afya,”
alisisitiza Munuo
Amesema kwmba, kwa tafiti
zilizofanyika hivi karibuni, tiba asili na dawa asili ndicho chanzo pekee
kinachoonyesha uwezo wa kutoa aina mpya ya dawa kwa matumizi ya sasa kwa
matumizi yajayo.
Munuo aliongeza kwa mujibu wa kitabu kilichoandaliwa na Wizara ya Afya
na Ustawi wa Jamii pamoja na Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala “TIBA ASILI
KWA JAMII mwezi Aprili mwaka 2009 kinasema kibiashara, soko la dawa za asili
duniani kwa mwaka 2004 lilikuwa dola za kimarekani bilioni 60.
Amesema kwa sasa inakadiriwa kufikia mwaka 2050 soko la Tiba Asili na
Tiba Mbadala litakuwa dola za kimarekani trilioni 5 na hapo ndio utaona mchango
wa tiba asili kwenye uchumi wa dunia.
Aliongeza kuwa sifa za kusajiliwa ni lazima mtu awe na umri wa miaka 18
au zaidi na anatoka katika familia ya mganga au mkunga ambako atakuwa amepewa
mafunzo ya uganga au ukunga wa tiba asili na siyo vinginevyo.
Kwa mujibu wa Dkt Othman Shem kutoka Paseko Natural Health Clinic
anasema kwamba Tiba Asili dnio tiba mama na kongwe kulio tiba zote duniani
iliyoanza kupambana na maradhi yanayo msumbua binadamu.
“Tiba asili huchangia matibabu ya binadamu duniani zaidi ya asilimia 60
hadi 80 hizi ni takwimu za Shirika la Afya Duniani,”
“kwa kusisitiza ni kwamba Tiba asili ndio chanzo cha tafiti nyingi za
madawa zinazofanywa na tiba zingine kama tiba mbadala na za kisasa,” amesema
Awali, Mwenyekiti wa ATME, Simba Abdulrahman Simba amesema kuna dawa
nyingi za tiba za asili ambazo zina matokeo mazuri kuliko inavyofikiriwa na
akaitaka Serikali kuruhusu dawa za jadi kutolewa hospitalini kama ilivyo nchi
nyingine duniani.
Mwanasheria kutoka AUDA, Onesimo Munuo (kushoto), akielezea mapungufu ya utekelezaji ya Tiba asili na mbadala |
Wahariri na waandishi kutoka vyombo mbalimbali waliohudhuria mafunzo hayo |
Mlezi wa Chama Cha Utabibu wa Dawa Asilia Tanzania (ATME), Kingunge Ngombale. Akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo |
Post a Comment