Ripoti
ya Jopo la Maendeleo ya Afrika ya mwaka huu inawahimiza viongozi wa
Afrika kupambana na ukosefu wa usawa na kuitaka jamii ya ulimwengu
kukabiliana na uporaji wa rasilimali za bara hili.
ABUJA, Nigeria, May 8, 2014 -- Rasilimali
za Afrika zenye utajiri mwingi zinatoa nafasi ya kipekee ya ufanisi
katika uimarishaji wa maisha ya raia wa Afrika, yasema ripoti mpya kubwa
iliyozinduliwa leo na Kofi Annan, Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa
Mataifa, lakini mara nyingi sana rasilimali hizi huporwa na maafisa
wafisadi pamoja na wawekezaji wa kigeni. Aidha, Ripoti hii inaonyesha
kwamba kuongezeka kwa ukosefu wa usawa vilevile kunaizuia Afrika
isiikamate nafasi hii ya maendeleo.
Post a Comment