Inasadikiwa kuwa mwanamke Charity Pierce, 38, anayeishi huko Iowa nchini Marekani ndiye mwanamke mwenye uzito mkubwa kuliko wote hapa duniani 765 lbs, (akimzidi yule wa hapa Arizona  -- Susanne Eman aliyekuwa na uzito wa paundi 756 mwaka juzi), amenuia kupunguza uzito ili aweze kufunga ndoa na mpenzi wake Tony anayempungua si tu kwa uzito na kimo bali pia umri wa miaka 17.

Wawili hao wamekuwa wapenzi tangu miaka mitatu iliyopita walipokutana kupitia urafiki wa binti wa Charity aitwaye Charly, 17, na tayari wameshachumbiana. Kwa sasa, Tony -- ambaye pia  ni kaka mdogo wa baba yake Charly -- anajitahidi kumpata daktari atakayemfanyia Charity upasuaji anaoamini utasaidia pia kuyaokoa maisha ya mpenzi wake na kisha kuwapa nafasi ya kufunga ndoa.

Tarehe 28 Machi 2014, timu ya Barcroft Tv walifika nyumbani kwake huko Cedar Rapids, Iowa na kuchukua picha za video na kutoa maelezo yake kama inavyoonekana katika video ifuatayo...





Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.