DEREVA wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani
Singida Juma Juma (52) amefariki dunia wakati akifanya mapenzi na mwanamke mhudumu
wa baa kwenye nyumba ya kulala wageni
.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida,SACP
Geofrey Kamwela amesema tukio hilo limetokea mei tatu mwaka huu saa nane za
usiku chumba no.S.2 nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Top Life
New Kiomboi mjini.
Amesema siku ya tukio,dereva Juma saa sita za usiku
alimwaga mpangaji wake kuwa anatoka mara moja na hatachelewa kurudi nyumba kwa
kwa hiyo alifunga mlango wa mbele ya nyumba.
Amesema kuwa saa mbili baadaye Juma alionekana akiwa
baa iliyoko kwenye nyumba hiyo la kulala wageni iliyoko umbali wa mita 50
kutoka nyumbani kwake.
"Muda huo Juma alionekana akiwa na mmoja wa wahudumu
wa baa hiyo alitwaye Agness Mayo (32) anayesadikika kuwa na uhusinao wa
kimapenzi na Juma.",amesema.
Kamwela amesema mhudumu huyo wa baa mpenzi wa
Juma,alitoweka mei nne mwaka huu baada ya kuaga kwamba anakwenda kanisani na
kutorokea kusikojulika.Hata hivyo,ufunguo wa chumba alicholala Juma zilikutwa
chumba cha kulala wahudumu wa baa.
Kamanda huyo amesema kuwa toka siku hiyo ya mei tatu
chumba alicholala Juma hakifunguliwa hadi mei tano mwaka huu na ndipo mwili wa
dereva huyo ulipokutwa ukiwa umeharibika vibaya.
"Uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea ikiwa
ni pamoja na kutafuta mhudumu aliyetoroka ili ahojiwe na kisha kufikishwa
mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili endapo atabainika kuhusika na tukio
hilo",amesema Kamanda Kamwela.
Post a Comment