KAMPUNI ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Shanta Mining Ltd imetoa leseni tatu na mtaji wa shilingi milioni 40 kwa kikundi cha wachimbaji wadogo cha Aminika cha kijiji cha Mang’onyi Wilayani Ikungi, Mkoani Singida.
Kikundi hicho Aminika Gold Mine Co-
Operative Society Ltd Mang’onyi, kimekabidhiwa leseni hizo hivi karibuni na
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stepheni Maselle kwenye kijiji cha Sambaru.
Akikabidhi leseni hizo Naibu Waziri Maselle
amewataka wanakikundi kujipanga vizuri katika kuanza kufanya kazi ya uchimbaji
dhahabu ili kujikwamua kimaendeleo.
Aidha amesema ni matarajio yake kuona kuwa
kikundi hicho kinakuwa na maendeleo na kuwa mfano wa kuigwa hapa nchini kwani
tayari nguvu kazi wamepewa mtaji na Shanta.
“Ndugu zangu sijui Mungu awape nini mmepewa
leseni, mmepewa mtaji na vifaa vya kuanzia kazi na hawa wenzetu wa Tan
Discovery mnaoneshwa eneo ambalo tayari limefanyiwa utafiti, sasa kazi kwenu.”
Amesema Maselle huku akishangiliwa na wananchi.
Aidha aliwataka wanakikundi hao kutumia
kama SACCOS katika kukopa sehemu mbalimbali za kifedha kwa manufaa yetu na
kizazi cha baadae.
Hata hivyo Naibu Waziri, Maselle amesema
ni dhamira ya serikali kuendeleza wachimbaji wadogo hapa nchini kwa kuwapatia
mafunzo na namna bora ya uchimbaji madini.
Katika risala ya wanakikundi cha Aminika
iliyosomwa na Katibu wake, Hamis Kingi amesema kikundi hicho ni muungano wa vikundi vitano kutoka vijiji vitatu vitakavyoathirika na Mgodi wa Kampuni
ya Shanta Mining vyenye jumla ya wanachama 218.
Kingi alivitaja vikundi hivyo kuwa ni
Elimika Sambaru,Amani Sambaru, Amka
Sambaru, Aminifu Mang’onyi na Muungano Mlumbi ambavyo kwa pamoja
vimeungana na kuwa kikundi kimoja kinachojulikana
kwa jina la Aminika
Aidha alitanabaisha kwamba vikundi baada ya maelekezo hayo
ya Serikali wachimbaji waliendelea kujiunga pamoja na kuunda kikundi kilichofuata utaratibu wa kisheria wa
kusajiliwa na kupata usajili namba, SIR624
Kikundi cha Aminika Gold
Mine Co – Operative Society Ltd – Mang’onyi hatimaye
wamekabidhiwa rasmi na Serikali.
“Mh,Naibu Waziri wa Nishati na Madini kwa kuwa
kikundi kiko Kisheria tunaomba
Serikali kupitia Wizara yako ya Nishati na Madini Makubaliano
yetu kati ya Kampuni na Kikundi cha
Aminika yaweze kutekelezeka kwa
muda mwafaka, kwani wanakikundi
wanahitaji kufanya kazi ili kujikwamua kiuchumi.”Alifafanua Kingi.
“Pia tunakushukuru wewe binafsi kwa juhudi zako kubwa kuwatetea wachimbaji wadogo kwa kupitia Wizara ya
Nishati na Madini.” Amesema.
Post a Comment