WATANZANIA taratibu wameanza kuona kama ni mchezo wa kuigiza au mazoea pale kila baada ya muda fulani tukio la kulipuka kwa bomu katika kanisa au sehemu ya mkusanyiko au kwenye mkutano wa kisiasa kama ni jambo la kawaida.
Imefikia mahali kwamba milipuko ya mabomu inaanza
kuonekana kama ni sehemu ya utamaduni wetu kwa kukubali kwa kirahisi watu wenye
dhamira ovu na katili ya kutaka kuangamiza binadamu wenzao pasipo sababu ya
msingi na hata kama mtu ana sababu ya msingi kuelezea hisia zake juu ya jambo
fulani lakini si kwa njia ya kutoa roho ya mtu mwingine.
Imekuwa kama mazoea kwa baadhi ya makundi ya watu
kutumia imani (dini) kuelezea hisia zao kali kwa kushambulia sehemu ya imani
nyingine hii kwa kweli kwa jamii iliyostarabika haikubaliki hata kidgo tena kwa
watanzania waliozoea kuishi pamoja bila kujali tofauti zao za rangi, dini,
kipato, itikadi au tofauti zozote wamekuwa wamoja tangu uhuru.
Na ndugu msomaji watanzania hawa wamekuwa wamoja
tangu enzi na enzi na waasisi wa taifa hili yaani Baba wa taifa, Mwl Julius
Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume waliweza kwa nguvu zao zote kuwaunganisha
watanzania na kuwa kitu kimoja bila mifarakano yoyote ndani ya jamii.
Sisi Moblog tunapenda kuchukua nafasi kuwaambia
watu, mtu au kikundi cha watu au magaidi kwamba watashidwa kwa nguvu ya dola na
mwenyezi mungu kwa mipango yao ya kiovu kutaka kutoa roho za watu wasio kuwa na
hatia.
Lakini kama kuna kikundi cha watu kinajificha kwenye
kichaga cha imani kutaka kuelezea hisia zao kwa kuwaua watu wengine yaani watu
wenye misingi au imani kali za kidini(Religious Fanaticism) kwa kweli ni upofu
wa kutokuona mbali kabisa lakini vyombo vya dola lazima viwajibike haraka na kuwashughulikia
kwa ukamilifu vikundi au kikundi kama hivi hapa nchini.
Tunasema mapema kwa kuvikumbusha vyombo vya dola kwa
sababu imani kali za kidini zikiachwa
kama ule msemo usemao ‘mchelea mwana kuliwa matangani’ kama kule Nigeria ambapo
kilundi cha kigaidi cha Boko Haram kinavyowatesa wananigeria na viongozi wao.
Tumesema hayo tukijua kwamba juzi tu mtu mmoja
amejeruhiwa baada ya kulipukiwa na kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu kwemye
kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini
Mashariki Ziwa Victoria, Makongoro Misheni, Mwanza.
Ambapo aliyejeruhiwa ni mhudumu wa nyumba ya wageni
ya kanisa hilo, Benadeta Alfred (25) aliyekubwa na mkasa huo juzi saa mbili
usiku.
Huo ukiwa ni muendelezo wa matukio kama hayo katika
sehemu mbalimbali hapa nchini hususani jijini Arusha chonde chonde Jeshi la
Polisi nchini chukueni hatua mapema ya kudhibiti hali hii isifike mahali
tukajuta kama nchi na watu wake.
Post a Comment