Akifafanua Gatambi
amesema mradi wa majaribio utaanza na mabasi 20 yatakayokuwa na uwezo wa
kuchukua abiria kati ya 145 hadi 160 kwa wakati mmoja hali itakayosaidia
kuondoa kabisa kadhia ya usafiri kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam.
DART kuanza kutoa huduma mapema mwakani
SERIKALI inatarajia
kuanza kutoa huduma za awali (interim services) katika mradi wa Mabasi yaendayo
Haraka (DART) Kutoka Kimara mwisho hadi Kivukoni jijini Dar es salaam mwaka
2015 baada ya miundombinu kukamilika.
Hayo yamesemwa na
Meneja Uhusiano wa Wakala wa mabasi yaendayo haraka (DART) Bw.William
Gatambi wakati wa mkutano na waandishi
wa habari hivi karibuni jijini Dar es salaam.
Gatambi amesema
kuwa mara baada ya kukamilika kwa miundo mbinu ya mradi huo awamu ya kwanza
mwishoni mwa mwaka 2014 itasadia kufanikisha usafiri wenye tija kwa wakazi wa
jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake.
Miundombinu hiyo,
inajumuisha barabara ya kilomita 20.9 kuanzia Kimara Mwisho hadi
Kivukoni,Barabara ya Kawawa kutoka Morocco hadi Magomeni na Barabara ya
Msimbazi hadi eneo la Gerezani Kariakoo.
Aliongeza kuwa ina vituo vidogo 27,vituo vikuu
vitano, vituo mlisho vine na karakana mbili. Pia inajumuisha njia za waenda kwa
miguu na baiskeli.
Aidha, katika mradi
huo wa majaribio Gatambi amesema kutakuwa na mabasi mengine 10 yenye uwezo wa
kuchukua abiria kati ya 50 na 60 ambayo yatatumika kuchukua abiria kutoka
pembezoni mwa jiji la Dar es salaam kuja katika vituo vikuu vya mabasi yaendayo
Haraka.
Kwa upande
wakeMeneja Usimamizi wa Barabara wa DART Mhandisi Mohamed Kuganda amesema mradi
huo utasaidia kuondoa tatizo la foleni Jijini Dar es salaam na kuwafanya
wananchi kupata huduma ya usafiri yenye kukidhi viwango vya Kimataifa.
Pia Kuganda amesema
DART kwa kushirikiana na Halmashauri za Jiji la Dar es salaam inafanya
maandalizi ya kuboresha barabara mlisho (feeder roads) katika maeneo
yatakayotumiwa na mabasi mlisho.
Katika mradi wa
mabasi yaendayo haraka kutakuwa na Vituo Vikuu (terminals) vitano 5 katika,
maeneo ya Kimara, Ubungo, Morocco, Kariakoo na Kivukoni ambapo vituo hivi ndiko
mabasi yatakapokuwa yanaanzia na kumalizia safari kubadilishana abiria kati ya
njia kuu na njia mlisho (feeder roads) ambapo vituo hivyo vikubwa vinatoa
nafasi ya kuweza kuanzishwa kwa huduma muhimu kwenye vituo hivyo kama maeneo ya
kukatia tiketi na vyoo.
Post a Comment