Dodoma. Kwa maneno ya siku hizi ni kwamba
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Fredrick Werema ‘amelikoroga na
kulinywa mwenyewe’, baada ya jana kutoa kauli ya kuudhi alipomtaka
mbunge kutoka Zanzibar akaulize swali lake visiwani humo, iliyosababisha
baadhi ya wabunge kususia Bunge na kutoka.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Fredrick Werema.PICHA|MAKTABA |
Kauli iliyoonyesha kuwagawa wabunge katika mafungu
mawili; wa bara na Zanzibar, ilimlazimu Jaji Werema baadaye kusimama
bungeni na kuwaangukia akiwaomba radhi waliokerwa na kauli yake na pia
kuliomba radhi Bunge, Spika wake, Anne Makinda na wananchi.
Kuondoka kwa wabunge hao kulitokana na mwongozo wa
Spika ulioombwa na Mbunge wa Ole (CUF), Rajabu Mbarouk Mohamed kutokana
na majibu Jaji Werema kwa mbunge wa Mkanyageni (CUF), Habibu Mnyaa
aliyekuwa ameomba ufafanuzi wakati Bunge lilipokaa kama kamati ya
kupitisha vifungu vya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya
Katiba na Sheria kwa mwaka 2014/15.
Mnyaa alisema Wizara ya Katiba na Sheria ni muhimu
lakini imekuwa ndiyo ya kwanza kuvunja sheria na haki za binadamu na
akataka ufafanuzi.
Hata hivyo, aliposimama kujibu swali hilo, Jaji
Werema alimwambia Mnyaa kuwa mambo mengine akaulize Zanzibar na siyo
katika Bunge la Jamhuri kwa kuwa si kila kitu kitaulizwa ndani ya Bunge
hilo.
“Alichokizungumza Mnyaa ni sahihi lakini hapa si
mahali pake, namshauri kuwa akaulize huko Zanzibar kwenye vikao vyao
hapa sisi hatuna majibu,” alisema Werema.
Mara baada ya Bunge kurejea, Mbarouk aliomba mwongozo wa Spika akitaka ufafanuzi wa kauli hiyo kwamba ilikuwa ya kibaguzi.
“Mheshimiwa Spika, huu ni ubaguzi na haupaswi kufanywa na mtu msomi kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali,” alisema Mbarouk.
Alisema ubaguzi huo umewabagua wabunge ambao
wamekula kiapo cha kulitumikia Bunge la Jamhuri ya Muungano na
unaonyesha namna ambavyo Wazanzibari wanabaguliwa.
“Mheshimiwa Spika, yanapofanyika mambo kama hayo
na wewe mwenyewe uko hapa unaona ni sawa na kubariki jambo hilo, huu ni
ubaguzi unaoufanya wewe kwa kuwa lilifanyika ukiona bila hata ya
kukemea,” alisema Mbarouk.
Hata hivyo, Spika alipinga na kusema: “Hakuna
mwongozo wowote kwa kuwa hata wewe umevunja sheria kwani hata
nilipokuambia kaa chini umeendelea kuzungumza, tunaendelea.... Katibu
(akimtaka Katibu wa Bunge kutoa mwelekeo wa shughuli iliyokuwa inafuata
ambayo ilikuwa Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi).”
Baada ya kauli ya Spika, wabunge wa Zanzibar
walihamasishana na kuamua kutoka nje kwa wakati mmoja na huku wenzao wa
upinzani wakiendelea kutafakari cha kufanya. Wakati huo, Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe alikuwa akisoma hotuba yake.
Muda mfupi baadaye, wabunge wa Chadema na NCCR Mageuzi nao walitoka na katika viti vya upinzani, alibaki John Cheyo wa UDP peke yake.
Baada ya kutoka
KULINYWA
“Mimi ni Jaji kwa taaluma na kwa nafasi yangu nimekosea kwa kutoa maneno hayo. Nimetambua kosa langu na naomba radhi... kwanza kwako Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rajab Mbarouk, Mheshimiwa Injinia Habib Mnyaa, Bunge hili na Watanzania kwa jumla.”
Chanzo cha habari na gazeti huru la kila siku la www.mwananchi.co.tz
Muda mfupi baadaye, wabunge wa Chadema na NCCR Mageuzi nao walitoka na katika viti vya upinzani, alibaki John Cheyo wa UDP peke yake.
Baada ya kutoka
Akizungumza nje ya Viwanja vya Bunge, Mbarouk
alisema wametoka kwa sababu Spika na Jaji Werema wamewadharau.
“Hatutarejea ndani ya Bunge hadi hapo watakapotuomba radhi, wasipotuomba
radhi hatutarejea bungeni,” alisema Mbarouk.
Hata hivyo, wakiwa nje ya Ukumbi wa Bunge, mbunge
wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed aliwafuata na kuwaeleza kuwa
amezungumza na Werema na amekubali kuomba radhi kwa wabunge na
Watanzania.
“Ndugu zangu nimeongea na Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, amekubali kuomba radhi,” alisema Hamad Rashid jambo ambalo
liliungwa mkono na wabunge wa CUF waliokuwa wamekaa katika makundi
katika Viwanja vya Bunge.
Hata hivyo, wabunge hao baada ya muda wa dakika
15, walikwenda katika kikao cha dharura kwenye Ukumbi wa Kambi ya
Upinzani ambako pamoja na mambo mengine, walijadiliana kusudio la
kumuona Spika Makinda kumweleza mambo yasiyowaridhisha.
Werema aomba radhi
Muda mfupi kabla ya Bunge kuahirishwa, Jaji Werema
alisimama na kusema: “Kwa imani yangu, ninaamini kila binadamu ana
nyongo, isipokuwa watu wawili... Yesu Kristo na Mtume Muhammad (SAW),
ndiyo pekee ambao hawakuwa na nyongo. Naomba maneno yangu yafutwe katika
kumbukumbu za Bunge hili.
“Mimi ni Jaji kwa taaluma na kwa nafasi yangu
nimekosea kwa kutoa maneno hayo. Nimetambua kosa langu na naomba
radhi... kwanza kwako Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rajab Mbarouk,
Mheshimiwa Injinia Habib Mnyaa, Bunge hili na Watanzania kwa jumla.”
KULIKOROGA
“Alichokizungumza Mnyaa ni sahihi lakini hapa si
mahali pake, namshauri kuwa akaulize huko Zanzibar kwenye vikao vyao
hapa sisi hatuna majibu.”
KULINYWA
“Mimi ni Jaji kwa taaluma na kwa nafasi yangu nimekosea kwa kutoa maneno hayo. Nimetambua kosa langu na naomba radhi... kwanza kwako Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rajab Mbarouk, Mheshimiwa Injinia Habib Mnyaa, Bunge hili na Watanzania kwa jumla.”
Chanzo cha habari na gazeti huru la kila siku la www.mwananchi.co.tz
Post a Comment