WAKULIMA mkoani Singida wamehimizwa kujenga utamaduni wa kuwa waaminifu kwa kuuza mazao yao bila kuchanganya na vitu vingine kuongeza uzito kwa madai kwamba vitendo hivyo vinaharibu masoko na kushusha thamani ya mazao.


 Wito huo umetolewa hivi karibuni na Meneja Masoko na Usambazaji wa Wakala wa Mbegu za Kilimo wa Taifa (ASA), Philemon Kawamala wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wakulima viongozi wa wilaya ya Mkalama mkoani Singida.


 Amesema baadhi ya wakulima wamekuwa sio waaminifu wakati wa kuuza mazao yao kwa kuchanganya mazao na vitu vingine kwa lengo la kuongeza uzito ili waweze kupata kipato zaidi.


Kawamala amesema kwa sasa wanunuzi wamekuwa wakitumia vifaa vya hali ya juu kupima na kuchunguza kwa kina mazao kabla ya kuyanunua.

Akifafanua zaidi,amesema baadhi ya wakulima hao huchanganya mazao yao ya biashara na mawe,vitu vichafu na baadhi ya wasindikaji mafuta nao huchanganya mashudu na udongo wa mbugani.


 “Kutokana na hatua hiyo ya upimaji, wakulima wamekuwa wakiumbuka kutokana na kutokuwa waaminifu.  Mazao yao hukosa sifa na kutokununuliwa kabisa kwa hiyo mkulima husika kuingia hasara na hivyo kurudisha nyuma maendeleo yake”,amesema.


 Kutokana na  hali hiyo, Meneja huyo amewataka viongozi wa kiserikali, kisiasa na wataalam wa kilimo kuwahimiza zaidi wakulima wajenge utamaduni wa kuwa waaminifu kwa maana ya kutokuchanganya mazao na uchafu mwingine ili mazao yao yaendelee kukubalika katika masoko ya ndani na nje ya nchi.


 Aidha, Meneja huyo ameitaka kambi ya magereza iliyopo kijiji cha Singa wilayani Mkalama, kutumia shamba darasa lao kuwaelimisha na kuwafunza wananchi walioko jirani juu ya umuhimu wa umuhimu wa kujikita kwenye kilimo bora.


Kwa upande wake, Mkuu wa kambi hiyo, Inspector Juma Mkoma amesema kambi hiyo yenye mashamba ya ukubwa wa zaidi ya hekta 500, hawana trekta wanategemea  majembe ya kukokotewa na ng’ombe kitendo kinachochangia kusiwepo na ufanisi katika kilimo.
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.