Mabingwa wa zamani wa Uingereza timu ya Manchester United imemteua kocha wa timu ya Uholanzi, Mhohalanzi Louis Van Gaal kama kocha wao mpya kuanzia mzimu ujao wa 2014/2015 kwa kumpa mkataba wa miaka mitatu akiwa anachukua nafasi iliyokuwa imeachwa wazi na laiyekuwa kocha wa timu hiyo David Moyes aliyetimuliwa mwanzoni wa mwezi wa tano.
Kocha wa timu ya Uholanzi kwa sasa, Luois van vaal

Louis Van Gaal (LvG ) amewahi pia kufundisha klabu maarufu duniani za nchi za Uhispania, Ujerumani na nyuimbani kwao na kuzipa mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kutwaaa mataji mbalimbali makubwa duniani ikiwamo ubingwa mara mbili wa klabu bingwa ya Ulaya kwa timu ya Ajax Amsterdam ya nchini Uholanzi na pia itakumbukwa ndio aliyevumbua vipaji mbalimbali vya mastaa waliowahi kuwika na wanaondelea kuwika kwa sasa kama Arjen Roben anayekipiga kwa sasa na mabinwa wa Bundesliga, Bayern Munich.

LvG amemteua pia mchezaji aliyepata umaarufu mkubwa na kwa kuichezea timu yake hiyo mppya, Ryan Giggs kama kocha msaidizi akiwa pia amewateua wasaidizi wake Frans Hoek ambaye kwa sasa ndiye kocha wa makipa wa timu ya taifa ya Uholanzi na mabaye atakumbukwa kwa kukuza vipaji vya makipa hodari kama Edwin van der Sar na kipa wa Barcelona wa sasa Victor Valdes. 

Pia atakuwemo Marcel Bout ambaye amebobea katika kusaidia kusoma timu pinzani kabla ya mchezo na ambaye amepata kufanya kazi na timu kama Bayern Munich, Telstar, AZ, FC Volendam na Feyenoord.
Kocha mteuliwa wa timu ya Manchester united, Louis van Gaal
















































Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.