KAMPUNI ya Saruji ya Tanga (TCCL) kupitia Bodi yake Wakurugenzi imeidhinishga gawio la hisa la shilingi za kitanzania bilioni 7 kwa wanahisa wake baada ya kupata faida ya shilingi bilioni 32,456,234 kwa mwaka 2013.
Akizungumza wakati wa Mkutano
wa 20 wa Mwaka wa Wanahisa wa kampuni hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,
Lawrence Masha alisema katika kipindi cha mwaka jana kampuni ya Tanga cement
iliweza kutimiza baadhi malengo muhimu na mafanikio katika utekelezaji wa
mkakati wake wa kuishi kufuatana na chapa yake na ahadi yake ya kuwa kivutio
cha taifa.
“Bodi
imependekeza gawio la shilingi 60 kwa kila hisa kwa mwaka 2013, (2012
ilikuwa shs 55) ikipelekea kiasi cha jumla kwa gawio la shilingi za
kitanzania bilioni 3.3 na hii inaleta gawio la jumla kwa mwaka la shs 110 kwa
hisa (2012 ilikuwa shs 100) hivyo kufanya jumla ya shs bilioni 7
kwa mwaka mzima,”
“Tunayo
fahari kwa mchango wetu kwenye maendeleo ya Tanzania na muhimu zaidi kwa maisha
ya watu wengi ambayo tunaweza kuyagusa na kuyaboresha kutokana na shughuli zetu
za biashara,” alisema Masha.
Akizungumza
changamoto zinazoikabili sekta ya biashara ya saruji nchini, mwenyekiti huyo
aliendelea kuelekeza kilio chao cha muda mrefu sasa dhidi ya saruji
inayoingizwa nchini bila kufuata taratibu za sheria za nchi
Masha
alilisitiza umuhimu wa serikali kuingilia kati na kuzuia uigizaji wa saruji kwa
njia za panya kwa sababu inaua soko kwa watengenezaji wa saruji wa ndani,
kuleta bidhaa ambazo zipo chini ya kiwango na pia kuinyhima serikali pato
litokanalo na kodi.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Cement, Reinhardt Swart alisema
kwamba mwaka jana uchumi wa Tanzania ulikua kwa asilimia saba ukachochea zaidi
maendeleo ya kiuchumi ndani ya nchi.
“Mahitaji
ya saruji kwa nchi jirani pia yalibaki kuwa juu na kupanua wigo kwa kampuni
katika kusambaza bidhaa hizo katika nchi za Rwanda, Burundi, Malawi na Jamhuri
ya Kidemokrasi ya Kongo,” aliongeza
Aliahidi
kwamba kampuni ya Tanga cement itaendelea kusaidia jamii kwenye maeneo ya afya,
elimu, maendeleo ya jamii na mazingira na kwa mwaka jana pekee walitumia kiasi
cha shilingi milioni 324 kwenye miradi mbalimbali ya jamii.
Post a Comment